PORTUGAL

Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno anatazamiwa kuzikwa leo jumatatu

Wachezaji wa zamani nyota wa Brezilia, ikiwa ni pamoja na mfalme wa kabumbu Pelé, mrithi wake Zico “Pele blanc” au Luiz Felpe Scolari, meneja wa klabu ya Seleçao iliyotwaa kombe la dunia katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2002, wametoa salaamu zao za rambirambi kufuatia kifo cha mchezaji wa zamani nyota wa Ureno, Eusebio da Silva Ferreira, akijulikana kwa jina la “chui mweusi”, aliefariki jana asubuhi akiwa na umri wa miaka 71.

Matangazo ya kibiashara

“ Ninasikitika kufuatia kifo cha ndugu yangu, Eusebio”, hivo ndivyo alivyoandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya kifo cha “chui mweusi”, ambae alikua mchezaji nyota wa Porugal katika miaka ya 1966.

“Tulitokea kua marafiki ndugu katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1966 nchini Uingereza”, amesema Pelé, akiweka picha waliyopigwa wakiwa wawili katika michuano hio iliyochezwa nchini uingereza.

Katika mchuano huo wa kuwania mshindi katika kundi lilozishirikisha timu hizo, Ureno iliifunga Brezil mabao 3-1, ambapo mabao mawili ya liingizwa wavuni na Eusebio da Silva Ferreira.

Timu hio ilimaliza michuano hio ikijikuta ilichukua nafasi ya tatu.

Zico, mchezaji mwengine nyota wa Brazil,ambae alikua akivalia jezi nambari 10 mgongoni, ametoa pia salaamu za rambirambi kufuatia kifo cha mchezaji huyo nyota wa zamani wa Ureno, Eusebio.

“Niliwahi kupata fursa ya kucheza nae dakika chache katika warsha ya miaka 50 ya (mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujeremani Franz Beckenbauer), amesema Zico, akibaini kwamba anaifikiria familia ya marehemu, huku akiomba Mwenyezimungu apokeye mikononi mwake.

Meneja wa Brezil, Luiz Felipe Scolari anakumbuka jinsi walivyoanza na marehemu mawasiliano yao kupitia tovuti iitwayo Globo Sports, wakati alikua akiinoa klabu ya Portugal katiaka miaka ta 2003 hadi 2008.

Muilli wa Eusebio umewekwa tangu jana jumapili kwenye uwanja wa Luz mjini Lisbonne, ambako ni makao makuu ya klabu yake ya zamani Benfika.

Mchezaji huyo nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno, atazikwa leo jumatatu katika makaburi ya Lumiar, mjini Lisbonne.