LIGI KUU UINGEREZA

Klabu ya Arsenal ya kumbwa na hali ya sintofahamu baada ya kumkosa kwa kipindi cha miezi sita mchezaji wake nyota theo Walcott

Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Arsenal Theo Walcott, ambae anauguza jeraha la goti, alilolipata jumamosi, hataonekana uwanjani msimu wote unaosalia, na atakosekana katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2014, itakayochezwa nchini Brezil, imefahamisha klabu anayochezea ya Arsenal.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa liyotolewa na klabu ya Arsenal, Walcott atafanyiwa upasuaji hivi karibuni kweye goti lake la kushoto, na atakosekana uwanjani katika kipindi cha miezi sita, na hatapatikana katika michezo inayosalia msimu huu, ikiwemo michuano ya kombe la dunia.

Theo Walcott, ana umri wa miaka 24, na ni mshamuliaji nyota, na ni mchezaji wa kiungo wa Arsenal, hata katika timu ya taifa ya Uingereza anawika, baada ya kushirikishwa mara 36 katika michuano mbalimbali na kuingiza wavuni mabao 5.

Theo alipata jeraha hili, jumamosi wakati klabu yake ya Arsenal iliifunga Tottenham mabao(2-0).

“Taarifa hii inanivunja moyo, na ni pigo kwa Arsenal, na taifa kwa ujumla”, ameandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya twitter, mlinzi wa Arsenal.

“ Ni pigo kubwa kwa Arsenal na taifa nzima, kwani nina imani kua Theo Walcott angelitamba nchini Brazil”, amesema mchezaji wa kati wa zamani wa Arsenal,Ray Parlour kwenye Sky Sport.

Walcott, ambae anaonekana bado ana umri mdogo, hajacheza katika michuano ya kombe la dunia, hata kama aliwahi kushirikishwa katika michuano ya kombe la dunia ilichezwa nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Walcott alishakosekana uwanjani kwa muda wa miezi miwili, baada ya kukosekana katika mechi mbili za ushindi wa Uingereza dhidi ya Monténégro na Poland.

Kiungo wa Tottenham, Andros Townsend, kwa sasa ndie anachukua nafasi ya Theo Walcott.

Kukosekana kwa walcott, kumezua hali ya wasiwasi kwa Arsenal, baada ya kumkosa kwa muda wa mwezi mzima wa januari mchezaji kutoka Danmark, Nicklas Bendtner, wakati Olivier Giroud akiwa na ishara za uchovu.

Kutokana na hali hii inayoikumba Arsenal wakati huu, huenda klabu hio ikajikita kwa kuwatafuta wachezaji kutoka vilabi vingine.