LIGI KUU UINGEREZA

Manchester City yajinyakulia tiketi ya kuingia fainali

RFI

Katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza ambayo inaendelea, Manchester City imeifunga jana jioni klabu ya West Ham mabao 6-0. Alvaro Negredo ameingiza wavuni mabao matatu, huku Edin Dzeko akiingiza mabao mawili. Kwa sasa Manchester City imejipatia tiketi ya kuingia fainali katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Man City inachukua nafasi ya pili baada ya Arsenal, na inasubiri bila hofu yoyote mechi ya marudio tarehe 21 mwezi huu wa januari. Manchester City itacheza mechi hio ikiwa nyumbani.

Man City inajianda pia kujielekeza mjini Newcastle kutimuana vumbi na timu ya mji huo jumapili katika siku ya 21 ya michuano ya ligi kuu ya Uingereza.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo, Manchester City imedhibiti mchezo, na katika dakika ya 12 na 27, Alvaro Negredo alliona lango la Adrian San Miguel kwa kuingiza mabao mawili, huku Yaya Touré akingiza wavuni bao 1 katika dakika ya 49.

Katika kipindi cha pili, Man City ilikuja juu, na kuingiza bao la tatu kupitia mchezaji Negredo, na kabla ya kipenga cha mwisho, Edin Dzeko aliingiza mabao mawili.

Hata hivyo, Manchester United, ambayo imefungwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Sunderland, itacheza mechi ya marudio tarehe 22 januari kwenye uwanja wa Old Trafford, baada ya kushindwa mara 4 katika michuano ya ligi kuu.