LIGI KUU UINGEREZA

Mchambuliaji wa Tottenham Jermaine Defoe anunuliwa kwa kitita kikubwa cha pesa

RFI

Mchambuliaji wa kimataifa kutoka Uingereza anaechezea klabu ya Tottenham, Jermaine Defoe, atajiunga na klabu ya Spurs katika michuano ya klabu bingwa katika kanda ya kaskazini mwa Amerika, ifikapo tarehe 28 mwezi wa aprili, imefahamisha kwabu ya Spurs.

Matangazo ya kibiashara

“Nilishuhudia mambo mengi hapa na mashabiki wangu walikua kila mara wananiunga mkono”, amesema Jermaine Defoe, mchezaji nyota, ambae ana umri wa miaka 31, huku akiwa ameingizia Tottenham mabao 142 tangu aanze kuichezea klabu hii.

“Ntaichezeana klabu ya Spurs hadi ntakapotimiza miaka 35”, amesema Defoe.

“Ni fursa kubwa kwa Jermaine Defoe, na hio ilikua kila mara akiizungumzia katika maisha yake ya kabumbu”, amesema kocha wakeTim Sherwood. Tim amebaini kwamba Defoe, alifanya kazi kubwa kipindi chote aliyochezea Tottenham.

Defoe alipata mafunzo ya mpira kupitia klabu ya West Ham, na baadae alijiunga na Tottenham na kuichezea kipindi chote hicho hadi leo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, kandarasi hio ya Defoe kuichezea klabu ya Spurs kwa kipindi cha maika 5, itagharimu zaidi ya pesa za euros milioni kumi na mbili.