FIFA-2014

Shirikisho la soka duniani FIFA kutowa tuzo ya mchezaji bora duniani "Ballon d'or

Christiana Ronaldo, Franck Ribery, Lionel Messi
Christiana Ronaldo, Franck Ribery, Lionel Messi

Shirikisho la Soka Duniani FIFA inatarajia kutowa tuzo mbalimbali za mpira wa miguu, ikiwemo tuzo la mchezaji bora duniani. Wachezaji wa kimataifa kutoka Argentina, Lionel  Messi, Christiano Ronaldo wa Ureno na Franck Ribery ndio wanaowania nafasi ya mchezaji bora wa soka kwa mwaka 2013. 

Matangazo ya kibiashara

Ghafla ya utowaji wa tuzo hizo unatarajiwa kufanyika katika makao makuu ya shirikishjo la soka duniani FIFA yaliyopo Zurich Uswisi.

Mchezaji wa Kimataifa wa Ureno Christiano Ronaldo na anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Real Madrid ya Uhispania ni miomgoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kutajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013 na kuchukua nafasi ya lionel Messi aliyeshinda taji hili mara nne.

Mbali na Ronaldo wachezaji wengine wanaopopewa nafasi ya kutwa taji hilo ni pamoja na Lionel Messi wa Barcelona, na frank Ribery wa Bayern Munich.
Mwaka uliopita ulikuwa mzuri sana kwa Christiano Ronaldo aliyeifungia Real Madrid mabao 69 katika mechi 59.

Aliyekuwa kocha wa Manchester United Sir Alex Furson, kocha wa bayern Munich Jupp Heynckes na Kocha wa sasa wa Borrusia Dortumond Jurgen Klopp ni miongoni mwa wale wanaowania taji la kocha bora wa mwaka.