UGANDA- CHAN

Uganda yashinda katika michuano ya CHAN

RFI

Timu ya taifa ya soka ya Uganda inayowashirikisha wachezaji wanaosakata kabumbu katika ligi za nyumbani iliifunga Burkinfaso mabao 2 kwa 1 katika mchuano wake wa ufunguzi wa michuano ya CHAN nchini Afrika Kusini. Vijana wa Kocha Milutin Micho walipata ushidni huo kupitia mchezaji Yunus Sentamu aliyefunga mabao yote mawili katika dakika ya 15 na 72 baada ya kuunganisha pasi safi kutoka kwa Francis Olaki aliyeingia katika kipindi cha pili.

Matangazo ya kibiashara

Katika bao la kwanza Yunus aliwapiga chenga mabeki na kipa na kufunga bao murua.

Cyrille Bayala aliipa Burkinafaso bao la kufutia machozi katika dakika ya 89 ya mchuano huo baada ya mabeki wa Uganda kufanya masihara.

Ushindi huu unaipa Uganda uongozi wa kundi la B kwa alama 3 ikifuatiwa na Morroco na Zimbabwe amabazo zina alama moja kwa kutoka sare ya kutofungana katika mchuano wao.

Katika mchuano wa leo, timu ya Ghana itaminyana na Congo-Brazzavile kwenye uwanja wa Free State Stadium, na baadae itafuata mechi itakayozikutanisha timu ya Libya na Ethiopia.

Kesho jumaine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itaminyana na Mauritania, huku Gabon Ikitamba uwanani na Burundi katka uwanja wa Peter Mokaba Stadium.