AFRIKA KUSINI-CHAN

Libya yajiandikishia alama 3 dhidi ya Ethiopia katika michuano ya CHAN

RFI

Mabao ya Abushnaf na Abdel Salam Omar yaliipa timu ya taifa ya Libya ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Ethiopia katika mchuano wa kundi C kinyangayiro cha CHAN kinachoendela nchini Afrika Kusini. Libya wanashriki katika michuanio hii ya CHAN kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 2009 nchini Cote d'Ivoire, lakini Ethiopia iliyoonesha soka safi katika michuano ya kuwania taji la taifa bingwa barani Afrika mwaka uliopita ikishiriki katika michiano hii kwa mara ya kwanza.

Matangazo ya kibiashara

Kipindi cha pili cha mchuano huo Ethipia walionesha mchezo wa kusisimua wakiimbiwa na mashbaiki wao waliofurika uwanajani.

Katika mchuano mwingine wa kundi hilo Ghana iliifunga Congo Brazavile bao moja kwa bila.

Kundi la C sasa linaongozwa na Libya ambayo ina alama tatu Ghana ni ya pili pia kwa alama 3, huku Congo na Ethiipia zikiwa za mwisho bila ya alama.

Leo, ni mechi za kundi D, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itamenyana na Mauritania kuanzia saa kumi na moja kamili jioni saa za Afrika ya Kati na baadaye Gabon watamenyana na Burundi saa mbili usiku saa za Afrika ya Kati .