BURUNDI-GABON-CHAN

Burundi na Gabon zatoka sare katika michuano ya CHAN

Timu ya taifa ya soka ya Burundi, ilitoka sare ya kutofungana na Gabon katika mchuano wake wa ufunguzi wa kundi D katika michuano ya CHAN inayoendelea nchini Afrika Kusini. Gabon ilipata nafasi nyingi za kupata mabao lakini safu ya ulinzi ya Intamba Murugamba ilikuwa imara na kuzuia mashambulizi kutoka kwa washambulizi wa Gabon.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Gabon ilipata bao katika dakika za lala salama lakini likakataliwa kwa sababu ya mshambuzi wake alikuwa ameotea.

Katika mchuano mwingine uliochezwa katuika uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane, mabingwa wa mwaka 2009 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walipata ushindi baada ya kuifunga Mauritania bao 1 kwa 0.

Bao hilo pekee la Leopard lilitiwa kimyani na Eddy Ngoyi Emomo katika dakika ya 50 ya mechi hiyo na sasa DRC inaongoza kundi la D kwa alama 3, ikifuata na Burundi na Gabon ambazo zina alama moja.

Leo mechi za Kundi A zinarejelewa tena katika uwanja wa Cape Town, Wenyeji Afrika Kusini watamenyana na Mali kuanzia saa kumi na moja na nusu saa za Afrika ya Kati, na baadaye Nigeria watamaliza kazi na Msumbiji kuanzia saa mbili usiku saa za Afrika ya Kati.

Kesho, Zimbabwe watachuana na Uganda, na baadaye Burkinafaso watamenyana na Morroco.

Timu ya taifa ya soka ya Burundi, ilitoka sare ya kutofungana na Gabon katika mchuano wake wa ufunguzi wa kundi D katika michuano ya CHAN inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Gabon ilipata nafasi nyingi za kupata mabao lakini safu ya ulinzi ya Intamba Murugamba ilikuwa imara na kuzuia mashambulizi kutoka kwa washambulizi wa Gabon.