BURKINA FASO-AFRIKA KUSINI-CHAN

Timu ya Burkina Faso imeanza kupoteza matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya CHAN

RFI

Michuano ya CHAN inayozishirikisha timu za taifa za wachezaji wa nyumbani inaendelea nchini Afrika Kusini. Burkina Faso imelazimika kwenda sare na Morocco ya bao 1-1.Bao la Burkina Faso limeingizwa katika dakika za lala salama. Bao hilo lililowekwa wavuni na Bassirou Ouedraogo katika dakika ya 88 ya mchezo huo liliwasaidia vijana hao wa Afrika magharibi kupata alama moja muhimu licha ya Morrco kupata bao la mapema katika dakika ya pili ya mchuano huo kupitia kwa Ibrahim El Bahri.

Matangazo ya kibiashara

Juhudi za Morocco kupata bao la pili ziligonga mwamba licha ya kuutawala mchunao huo kwa kipindi kirefu lakini El Bahri alikaribia kuwapa vijana hao wa Afrika Kaskazini bao la pili lakini bahati haikufana.

Katika mchuano mwingine wa kundi hilo, vijana kutoka Kampala uganda Crens walitoka sare ya kutofungana na ndugu zao kutoka Harare Zimbabwe katika mchuano uliochezwa mapema jana jioni katika uwanja wa Athlone.

Kwa matokeo hayo, Uganda wanaongoza kundi la B kwa alama 4, Morrcoco ni ya pili kwa alama 2 sawa na Zimbabwe.

Burkina Faso ambayo ni ya mwisho kwa alama 1 imeanza kupoteza matumaini ya kusonga mbele kwa sababu wanastahili kuishinda Zimbawe na kuomba kuwa Uganda wawafunge Morroco katika mchunao wa mwisho ili kuwa na matumaini ya kusonga mbele.

Leo, Ghana watamenyana na Libya, saa kumi na moja kamili saa za Afrika ya Kati na baadae Ethiopia watachuana na Congo brazavile, Kesho Jumamosi, Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo watachuana na Gabon katika mchuano wa kundi D, huku Burundi ikimenayana na Mauritania.