SOKA-CHAN

Ethiopia yaaga michuano ya CHAN huko Afrika Kusini

ethioabay.com

Nchi ya Ethiopia imebanduliwa nje ya michuano ya CHAN inayozishirikisha timu za taifa za wachezaji wa nyumbani katika bara la Afrika, Ethiopia imelazimika kufungasha virago vyake baada ya kichapo cha bao 1-0 toka kwa Congo kwenye mechi ya michuano hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Libya imeendelea kusalilia kileleni mwa timu za kundi C kwenye michuano hiyo inayoendelea kutimua vumbi nchini Afrika Kusini.

Sare ya bao 1-1 dhidi ya Ghana, iliiwezesha Libya kuendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi yao kwenye michuano hiyo.

Libya wana pointi 4 katika mechi 2 baada ya kuichapa Ethiopia 2-0 kwenye mechi ya ufunguzi kundi C.

Ghana pia wana pointi 4 wakiwa katika nafasi ya pili baada kuifunga Congo katika mechi yao ya kwanza.

Baada ya kuichapa Ethiopia, Congo ipo katika nafasi ya 3 ikiwa na pointi 3 mkononi.

Ghana watakutana na Ethiopia katika mechi ya mwisho ya kundi lao siku ya jumanne, lakini mchezaji muhimu wa Ghana Yahaya Mohammed hatoshuka dimbani.

Mchuano mwingine wa makundi ni kati la Libya na Ghana ambao nao watachuana siku hiyo hiyo.