LIGI KUU UINGEREZA

Mchezaji nyota kutoka Ufaransa Nicolas Anelka akabiliwa na mashtaka ya ubaguzi

Nicolas Anelka, mchezaji wa klabu ya West Bromwich Albion
Nicolas Anelka, mchezaji wa klabu ya West Bromwich Albion RFI

Nicolas Anelka raia wa Ufaransa, ambae anaichezea klabu ya Uingereza ya West Bromwich Albion ameshtakiwa jumanne hii na shirikisho la soka la Uingereza (FA) kwa ajili ya " ishara ya mikono ", aliyoonesha uwanjani,ambayo inaonekana kwa baadhi kama tendo la ubaguzi dhidi ya wayahudi. Anelka iwapo atakutikana na hatia atakabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kucheza mechi . Nicolas Anelka ana muda hadi alhamisi kujibu mashtaka dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

"Inaonekana kua Anelka alifanya ishara ya matusi, au uchafu, au tendo lisiyokua sahihi ", limetangaza shirikisho la soka la Uingereza katika taarifa yake. " Aidha, ni ukiukwaji mkubwa (...) ikiwa inamaanisha ishara za matusi katika baadhi ya makabila au dini au imani, "limeendelea kubaini tangazo hilo.

Mshambuliaji huyo kutoka Ufaransa, ambae ana umri wa miaka 34 sio mara ya kwanza anaonesha ishara hio ya mikono. Disemba 28, wakati alipokua akisheherekea goli lake alilolifunga dhidi ya West Ham alionesha ishara ya mikono kama ishara ya salaamu kwa rafiki yake Dieudonné,muigizaji wa Ufaransa, ambae ni muasisi wa ishara hio ya mikono.

Ishara hii - mkono wa kulia ao kushoto kuelekeza chini, na mwengine kugusa kwenye bega ni ishara ya matusi, ambayo ilisababisha uhasama nchini Ufaransa miaka iliyopita.

Baada ya wiki tatu na nusu ya uchunguzi uliyofanywa na mtaalam alieteuliwa na shirikisho la soka nchini Uingereza, shirika hilo limeamua kufungua mashtaka. Kamati huru inayoundwa na wajumbe watatu imeteuliwa kutatua suala hili.

Anelka ambae alijiunga na dini ya Uislamu mwaka 2004, sasa ana muda hadi Januari 23 saa 12:00 jioni saa za Uingereza kukubali au kupinga tuhuma dhidi yake. Kama atakubalika kosa, atachukuliwa hatua za kisheria papo hapo, na iwapo atapinga, ataitishwa baadae jujieleza mbele ya shirikisho la soka la Uingereza (FA).