Michezo

Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchuana kusaka tiketi ya kufika robo fainali -CHAN

Timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba
Timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba BILALI

Timu ya taifa ya Burundi Intamba Murugamba inashuka uwanjani baadaye leo jioni kuchuana na Leopards wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC katika michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani.

Matangazo ya kibiashara

Vijana wa Intamba mu Rugamba wanashuka dimbani kuchuana na Leopards wa DRCongo wakiwa na matumaini ya kufuzu kuingia katika robo fainali hiyo baada ya kuwashinda Mauritania mabao 3 -2 na kutoka sare ya kutofungana na Gabon.

Burundi inaongoza katika kundi D, iliojumuisha DRCongo, Mauritania, Gabon na Burundi.

Ushindi wa bao moja au sare ya aina yoyote inahitajika kwa Burundi ili kuvuka ngazi hiyo. wakati huo huo Gabon inatakiwa kuifunga Mauritania ili kuiachia njia Burundi kuingia katika robo fainali.

Mauritania tayari imefunga virago.