CAPITAL ONE

Manchester City yatinga fainali ya Capital one

kikosi cha klabu ya Mancester City
kikosi cha klabu ya Mancester City RFI

Klabu ya soka ya Uingereza ya Manchester City imetinga katika fainali ya michuano ya Capital One baada ya ushindi wa mabao 3 kwa 0 dhidi ya West Ham Jumanne usiku.  

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Manchester City yalitiwa kimyani na mshambulizi Alvaro Negredo aliyefunga mabao mawili huku, Sergio Aguero akifunga bao la ushindi.

Kwa ujumla Manchester City wamefuzu kwa mabao 9 kwa 0 baada ya kuifunga West Ham mabao 6 kwa 0 katika mchuano wa kwanza.

City sasa watamenyana na Manchester United au Sunderland wanaopambana katika mchuano wa nusu fainali ya pili Jumatano usiku kabla ya fainali kupigwa tarehe 2 Februari katika uwanja wa Wembley.

Katika mchuano wa kwanza, Sunderland waliwafunga Manchester United mabao 2 kwa 1 na wanahitaji kupata ushindi wa zaidi ya mabao 3 kwa 0 ili kuwa na matumaini ya kufika fainali.

United wanashuka dimbani bila ya nahodha wao Nemanja Vidic aliyefungiwa kucheza mechi tatu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Chelsea Eden Hazard mwishoni mwa juma katika mchuano wa ligi kuu ya soka nchini humo.

Patrice Evra naye ana jeraha, na washambulizi Wayne Ronney ambaye amekuwa akiuguza jeraha na Robin Van Persie huenda wakakosa mchuano wa Jumatano usiku.

Kocha wa Manchester United David Moyes alinukuliwa akisema juma hili kuwa licha ya vijana wake kushindwa kupata ushindi katika mchuano wa kwanza wana uwezo wa kubadilisha matokeo hayo na kuandikisha ushindi Jumatano usiku.