UJERUMANI-Ligi kuu

Bayern Munich itamkosa Frank Ribéry katika chuano wa hapo ijumaa

Mchezaji wa klabu ya Bayern Munich, Frank Ribéry huenda asichezi katika mchuano utakaoishirikisha klabu yake hapo ijumaa mjini Mönchengladbach, kutokana na jera la mguu, amethibitisha Kocha wa Bayern Muich, Pep Guardiola.

RFI
Matangazo ya kibiashara

“ Frank ana maumivu miguuni. Hatujafahamu bado iwapo atacheza”, amesema Guardiola, bila hata hivo kufahamisha ni aina gani ya jeraha linalomsumbua mchezaji wake. Hayo ameyafahamisha katika mkutano wa kawaida na waandishi wa habari kabla ya mkesha wa mchuano.

Hata hivo, Guardiola, amesema mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa alionekana mdhaifu baada ya kushindwa katika kinyang'aniro cha kuwania tuzo ya mpira wa dhahabu.

“Alipatwa na mfadhaiko mkubwa, kwa sababu alihitaji kunyakua tuzo ya mpira wa dhahbu, kwa hivyo amekua akifikiria kwa kipindi kirefu mkasa huo uliyomtokea katika msimu huo, lakini kila mara amekua na imani kua atashinda siku moja, amesema Guardiola.

Ribéry, mweye umri wa miaka 30 alikosa uwanjani mara tatu katika robo ya mechi za kwanza za michuano ya Ujerumani. Kabla ya mechi hizo, Frank Ribéry aliifungia klabu yake mabao 6 na kutoa pasi nzuri za uhakika.

Guardiola amesema kwamba Bastian Schweinsteiger, ambae amefanyiwa upasuaji kwenye mguu atasalia nyumbani, lakini Arjen Robben, ambae ameanza mazoezi leo, tangu apate jeraha kwenye paja, ataweza akajielekeza mjini Gladbach kushiriki mchuano.