KENYA-Riadha

Kodi ya leta utata kwa wanariadha nchini Kenya

Bingwa wa dunia wa mbio hizo za Marathon Wilson Kipsang
Bingwa wa dunia wa mbio hizo za Marathon Wilson Kipsang RFI

Wanariadha nchini Kenya wanatishia kutoiwakilisha nchi yao katika mashindano mbambali ya Kimataifa ikiwemo michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 ikiwa serikali itaanza kutekeleza mpango wa kuwataka waanze kulipa kodi.

Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa na wanaraidha Wesley Korir Bingwa wa mbio za Boston Marathon na bingwa wa dunia wa mbio hizo za Marathon Wilson Kipsang, wakimbiza upepo hao wanasema wanashangazwa ni kwanini serikali inawataka walipe kodi wakati wao wanafanya kazi kubwa ya kuliwakilisha taifa na kuliletea sifa.

Tume ya kukusanya kodi nchini humo KRA inasema wanaridha hao ni wafanyakazi na laizma walipe kodi kama wafanyakazi wengine, suala ambalo pia aliyekuwa waziri kuu Raila Odinga amesema sio sahihi kwa serikali kuwatoza kodi wanardiha hao kwa kile anachoeleza ni kama kuwakatisha tamaa vijana kuonesha vipaji vyao kimichezo.