SOKA-CHAN

Nigeria na Zimbabwe zatinga nusu fainali michuano ya CHAN

Nigeria na Zimbabwe zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya CHAN inayowashirikisha wanasoka wa barani Afrika wanaocheza ligi za nyumbani, Nigeria ilitoka nyuma na kufanikiwa kupata ishindi wa mabao 4 kwa 3 dhidi ya Morcoco katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Cape Town jana Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Hadi mwisho wa kipindi cha kwanza, Super Eagles walikuwa wamefungwa mabao 3 kwa 0 na Atlas Lion, katika kipindi cha pili Nigeria walifanikiwa kusawazisha mabao yote na hadi dakika 90 mabao yalikuwa sare ya mabao 3 kwa 3.

Mchuano huo uliingia katika muda wa ziada na makosa ya kipa wa Morroco yalimpa nafasi mshambuliaji wa Nigeria Aliyu Ibrahim kufunga bao la nne na la ushindi.

Nigeria sasa watacheza na Ghana, katika hatua ya nusu fainali siku ya Jumatano juma lijalo.

Zimbabwe ambao walipata uungwaji mkono kutoka kwa idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza uwanjani waliifunga Mali mabao 2 kwa 1 katika mchuano mwingine wa robo fainali jana usiku.

Zimbabwe sasa inasubiri mshindi kati ya Libya na Gabon ambao wanacheza katika mchuano mwingine wa robo fainali.

Leo Jumapili kutakuwa na michuano miwili ya robo fainali, katika mchuano wa kwanza, Gabon watamenyana na Libya katika uwanja wa Peter Mokaba, huku Ghana ikimenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja wa Free State.