LIGI KUU UINGEREZA

Uingereza : Manchester United yapata ushindi

Mshambulizi matata wa manchester United, Robin Van Persie
Mshambulizi matata wa manchester United, Robin Van Persie RFI

Baada ya klabu ya soka ya Uingereza Manchester United kumsajili Juan Mata, mabingwa hao wa zamani wa soka nchini Uingereza walipata ushindi wa manao 2 kwa 0 dhidi ya Cardiff City siku ya Jumanne. Mabao ya Manchester United yalitiwa kimyani na mshambulizi matata Robin Van Persie katika dakika ya sita ya mchuano huo, bao alilofunga baada ya kuwa nje ya uwanja wa soka kwa sababu ya jeraha ambalo limekuwa likimsumbua.

Matangazo ya kibiashara

Pasi murua ya Mata ilimpata Ashley Young aliyeipa united bao la pili kupitia kichwa kipindi cha pili cha mchuano huo.

Kabla ya ushindi wa jana usiku, United walikuwa wamefungwa nyumbani mara tatu lakini ushindi huu umepunguza alama walizo nyuma ya viongozi wa ligi kwa alama 12.

Viongozi wa ligi Arsenal walitoka sare ya mabao 2 kwa 2 na Southmpton, huku Libverpool wakiwachabanga watani wao wa jadi Everton mabao 4 kwa 0.

Mechi za ligi kuu zinaendelea leo Jumatano, Aston Villa watamenyana na West Brom, Chelsea wachuane na West Ham na Sunderland na Stoke.

Manchester City watakuwa ugenini kumenyana na Tottenham Hotspurs na ikiwa watapata ushindi watapanda kileleni mwa ligi kuu kwa alama 53 mbele ya viongozi Arsenal ambao sasa wana alama 52.