LIBYA-GHANA-CHAN

Libya na Ghana zakutana fainali

Wacheza wa timu ya taifa ya Libya wakisheherekea ushindi wao dhidi ya Zimbabwe, 29 desemba 2014
Wacheza wa timu ya taifa ya Libya wakisheherekea ushindi wao dhidi ya Zimbabwe, 29 desemba 2014 RFI

Libya itachuana na Ghana katika fainali ya kuwani taji la timu bora barani Afrika katika mchezo wa soka baina ya wachezaji wanaosakata kabumbu katika ligi za nyumbani baada ya kuibuka na ushindi katika michuano ya nusu fainali siku ya Jumatano usiku nchini Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Libya na Ghana wanakutana mara nyingine katika historia ya soka barani Afrika, mwisho walikutana mwaka 1982 katika fainali ya kombe la mataifa bingwa na Ghana kushinda kwa mikwaju ya penalti 7 dhidi ya 6 baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1.

Libya walifika fainali baada ya kuwashinda Zimbabwe katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali kwa mabao 5 kwa 4 baada ya kutoka sare ya kutofungana katika muda wa kawaida na muda wa zaidi.

Ghana nayo ilifuzu baada ya kuifunga Nigeria mabao 4 kwa 1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya kutofungana katika muda wa kawaida na muda wa ziada.

Wachambuzi wa soka wanasema kuwa michuano ya nusu fainali ilikuwa migumu mno kutokana na kila timu kutopata mabao katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

Nigeria ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hii sasa watamenyana na Zimabwe kutafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi katika mchuano wa kwanza kabla ya fainali katika uwanja wa Cape Town.

Ghana itaingia fainali ikiwa inajivunia wachezaji wenye uwezo wa kumiliki mpira na kukimbia kwa muda mrefu lakini Libya wanaelezwa kuwa na uwezo wa kucheza soka kwa utaalam mkubwa na kupiga pasi fupifupi.

Timu zote mbili zitakuwa zinatafuta nafasi ya kujiunga na DR Congo na Tunisia ambayo waliwahi kushinda taji hili katika historia ya michuano hii. Libya itachuana na Ghana katika fainali ya kuwani taji la timu bora barani Afrika katika mchezo wa soka baina ya wachezaji wanaosakata kabumbu katika ligi za nyumbani baada ya kuibuka na ushindi katika michuano ya nusu fainali siku ya Jumatano usiku nchini Afrika.