LIGI KUU UINGEREZA

Chelsea yailambisha mchanga Manchester City kwa bao moja kwa nunge

Ivanovic, mchezaji wa Chelsea aliewaliza mashabiki wa Manchester City
Ivanovic, mchezaji wa Chelsea aliewaliza mashabiki wa Manchester City RFI

Klabu ya Chelsea, imefanikiwa kwa mara ya kwanza kuiweka kimya Manchester City ikiwa nyumbani msimu huu kwa bao (1-0) jana jumatatu katika katika mechi ya siku ya 24 ya mzunguuko wa michuano ya ligi kuu ya Uingereza, bao ambalo limewekwa kimyani na Ivanovic katika dakika ya 32 ya mchezo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa timu hizi mbili ziko sawa alama, licha ya kushindana magoli. City ambayo imekua inaongoza katika ligi tangu jumatano juma liliyopita, sasa imeshuka na fasi ya pili baada ya kufungwa jana na Chelsea.

Furaha ni tele kwa klabu ya Arsenal ambayo ilikua nafasi ya pili, na imepanda ngazi na kujikuta inashikilia na fasi ya kwanza, baada ya kuibwaga Crystal Palace juzi jumapili kwa mabao (2-0).

City imenyamanzishwa ikiwa nyumbani, ikiwa ni mara ya kwanza tangu novemba mwaka 2010.

Baada ya kwenda sare ya (0-0) ikiwa nyumbani katika mchezo wake na West Ham, Chelsea imeonekana bingwa hapo jana baada ya kuiweka Machester City katika hali ya sintofahamu.

City inajiandaa kumenyana na Chelsea katika mechi ya marudiano itakayo chezwa mnamo majuma mawili, kabla ya kucheza na Barcelona katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Chelsea kwa upande wake inajiandaa kujielekeza katika mji wa Galatasaray.