OLIMPIKI

Michuano ya Olimpiki ya Sochi yazinduliwa rasmi nchini Urusi

Michuano ya Olimpiki ya msimu wa baridi imezinduliwa rasmi katika mji wa kitalii wa Sochi nchini Urusi. Rais wa Urusi Vladmir Putin ndiye aliyezindua michuano hiyo ambapo katika siku ya kwanza watu wapatao 40,000 walikuwepo uwanjani.

Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa mataifa 44 wamehudhuria ufunguzi wa michuano hiyo ambayo imevunja rekodi ya kuwa na gharama zaidi baada ya kugharimu dola bilioni 30.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais wa Kamati ya Olimpiki ya dunia, Thomas Bach amehimiza michuano hiyo itumike kuwaunganisha watu na kupiga vita ubaguzi.

Mwenge wa olimpiki uliwashwa na Vladislav Tretiak and Irina Rodnina wa Urusi ambao ni washindi mara tatu wa zamani wa medali za dhahabu.

Wanariadha wa Urusi wanashinikizwa na mashabiki wao kufanya vizuri zaidi ili kutwaa medali nyingi zaidi hada ukizingatia nchi yao inaandaa michuano hiyo kwa mara ya kwanza toka walipokuwa wenyeji kwa mara ya mwisho mwaka 1980.