SOKA-ULAYA

Chelsea yakaa kileleni ligi kuu Ulaya baada ya kuinyuka Newcastle United 3-0

Mshambuliaji wa Chelsea Hazard akipachika bao kwenye nyavu za Newcastle
Mshambuliaji wa Chelsea Hazard akipachika bao kwenye nyavu za Newcastle RFI

Timu ya Chelsea imefanikiwa kuchupa kutoka katika nafasi ya tatu hadi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu barani Ulaya baada ya kuichakaza vibaya timu ya Newcastle United kwa magoli 3-0 kwenye mtanange wa jana Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kwamba Manchester City lazima iendelee kuchukuliwa kama mabingwa wa ligi kuu licha ya kuona timu yake ikichupa hadi nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza tangu mwezi Septemba.

Chelsea imeonesha nia yao katika uwezekano wa kushinda kombe hilo katika msimu huu bada ya wiki ya mafanikio kwao baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Manchester City, kabla ya kuwachapa vibaya Newcastle United jana Jumamosi.

Aidha katika mtanange mwingine Arsenal imeichakaza Liverpool magoli 5-1 huku Manchester City ikiambulia sare tasa na Norwich City, na hivyo kuifanya Chelsea kukaa kileleni kwa sasa wakiwa wamesaliwa na michezo 13.