LIGI KUU UINGEREZA

Chelsea yatoka sare na West Bromwich Abion

Jose Mourinho, kocha wa Chelsea
Jose Mourinho, kocha wa Chelsea AFP/N.Asfouri

Baada ya kushikilia nafasi ya kwanza katika siku ya 25 ya michuano ya ligi kuu ya Uingereza inayoendelea, klabu ya Chelsea imeanza kupoteza nafasi hio, baada ya kutoka sare ya bao (1-1) na West Bromwich Albion katika siku ya 26 ya michuano hio hio jana.

Matangazo ya kibiashara

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, amebaini kwamba wachezaji wake walikua wamepuuzia mechi hio.

“Kwa kweli wachezaji walikua wamepuuzia mchuano dhidi ya West Bromwich Albion, na hali hio imesababisha tunapoteza alama, wakati tumekua na uwezo wa kushinda”, amesema Mourinho.

Mourinho amebaini kwamba hali hio aliona mapema wakati mechi hio imekua ikichezwa, huku akisema kwamba wachezaji wake wangeimarisha ngome yao, lakini sivyo ilivyokua, “kwani katika dakika 10 kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa, wachezaji wanaocheza kwenye safa ya ulinzi walizubaa, na kujikuta West Bromwich Albion inasawazisha, amesema akisikitika, kocha wa Chelsea”, Jose Mourinho.

Chelsea bado inaongoza katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza, ikiwa mbele ya Arsenal kwa alama mbili, na Manchester City kwa alama tatu.

“Mnamo dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika, West Bromwich Albion, wametutia tumbo joto hadi kua na wasiwasi, na ni afadhali hivi wametoka sare”, amesema Mourinho.