Michezo

Manchester United yaikwamisha Arsenal kupaa kileleni mwa ligi kuu nchini Uingereza kwa kuilazimisha sare ya bila kufungana

vijana wa timu za Arsenal na Manchester United
vijana wa timu za Arsenal na Manchester United

Klabu ya Arsenal hapo jana imeshindwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kulazimishwa sare ya  bila kufungana na Manchester United usiku wa jana na kujikuta imebaki kwenye nafasi ya pili kwa kutimiza pointi 56 baada ya kucheza mechi 26 sawa na Chelsea yenye pointi 57 kileleni.

Matangazo ya kibiashara

Manchester United yenyewe imejiongezea pointi moja na kufikisha 42 baada ya kucheza mechi 26 na inaendelea kukaa nafasi ya saba.

Mechi hiyo ilisubiriwa kwa hamu kubw ana mashabiki kutoka katika kila kona za dunia, wati Arsenal ilitakiwa kuhakikisha inaibuka mshinda na kurejea kwenye nafasi ya kwanza ya ligi kuu nchini Uingereza huku Manchester nayo ilihitaji kuendeleza ubabe dhidi ya Arsenal licha ya kuwa nyuma katika msimamo wa ligi kuu.

Wakati huo huo klabu ya Liverpool  imepanda hadi kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo baada ya kuifunga Fulhammabao 3-2 jana usiku.

Kolo Toure alijifunga dakika ya nane kuipatia Fulham bao la kwanza na Richardson akaifungia timu hiyo bao la pili dakika ya 63.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Daniel Sturridge dakika ya 41, Coutinho dakika ya 40 na mkongwe Steven Gerrard dakika ya 90 kwa penalti.

Liverpool sasa imetimiza pointi 53 baada ya kucheza mechi 26 na inabaki nafasi ya nne.