Michuano barani Afrika

Michezo iliyochezwa mwishoni mwa juma liliyopita barani Afrika

Kikosi cha wachezaji wa klabu ya Yanga African
Kikosi cha wachezaji wa klabu ya Yanga African RFI

Yanga FC ya Tanzania, Gor Mahia FC ya Kenya , KCC ya Uganda, Flambeau de l'Est ya Burundi na AS Vita Club zimefuzu katika hatua ya pili ya michuano ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika baada ya ushindi wa michuano ya mzunguko wa pili iliyochezwa mwiohsoni mwa juma liliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Yanga waliwashinda Komozorine Fc ya Comoros mabao 5 kwa 2 na kufuzu kwa jumla ya mabao 12 kwa 2.

Gormahia nao wakiwa nchini Gabon waliwashinda US Bitam mabao 3 kwa 1 kupitia mikwaju ya penalti, huku AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikafuuzu kwa kuishinda Kano Pillarsya ya Nigeria kwa jumla ya mabao 4 kwa 3.

Na kuhusu michuano ya kuwania taji la shrikisho barani Afrika, AFC Leopards ya Kenya, AS Kigali ya Rwanda , Don Bosco ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Al Ahly Shendi vimefuzu katoka mzunguko wa pili baada ya michuano ya mwoshoni mwa juma.

AFC ilishinda Defence ya Ethiopia nyumbani kwao mabao 2 kwa 1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4 kwa 1, AS Kigali ikafuzu Academie Tchite mabao 2 kwa 1 baada ya sare ya bao 1 kwa 1 jana jijini kigali.

Azam FC ya Tanzania imeondolewa katika michino hii baada ya kufungwa na Ferroviaro be Beira ya Msubiji mabao 2 kwa 0 ugenini.

AFC Leopards itamenyana na Supersport united ya Afrika Kusini nyumbani na ugenini, As Kigali na Al Ahly Shendi , CS Don Bosco ya DRC na Djoliba ya Mali, michuano ya awamu ya pili zitakazochezwa nyumbani na ugenini mwishoni wa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kuhusu michuano ya klabu bingwa barani Afrika, Yanga watamenyana na Al Ahly ya Misri, Gor Mahia na Esperenace de Tunis, Nkana ya Zambia na KCC ya Uganda huku Dynamos ikimenyana na Priemeiro de Agosto.