MICHUANO YA KLABU BINGWA / ULAYA

Michuano ya soka ya kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA yaanza kutifua vumbi

Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha klabu ya Manchester City
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha klabu ya Manchester City RFI

Mchuano unaosubiriwa kwa hamu kubwa usiku wa leo ni kati ya Manchester City ya Uingereza amabao watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad dhidi ya Barcelona ya Uhispania. Barcelona watakuwa ugenini wakitaka kupata ushindi baada ya kuondolewa katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Kocha wa Barcelona Mwaregtina Gerardo Martino  amesema kuwa anaiheshimu sana Manchester City ambayo inawachezaji kama Álvaro Negredo, David Silvana Jesús Navas wote kutoka Uhispania   lakini vijana wamedhamiria kuindoa Mancheter City katika michuano hii.

Naye Kocha wa Manchester City Manuel Pelelegrini amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wacheze kwa kasi na kushambulia zaidi ili kupata bao la mapema.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambaye zamani alikuwa kocha wa Real Madrid na kuwa mpinzani mkubwa wa Barcelona yeye anasema kuwa kiwango cha Barcelona kimeshuka na Manchester City ina nafasi kubwa ya kutwa ushindi katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad.

Katika mchuano mwingine leo usiku, Bayer Leverkusen ya Ujerumai watakuwa nyumbani dhidi ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Kesho Milan ya Italia itachuana na Atletico Madrid ya Uhispania, huku Arsenal ya Uingerewa wakiwa nyumbani dhidi ya Bayern Munich wa Ujerumani.