Michuano ya Klabu bingwa Ulaya UEFA

Barcelona yaishinda Mancheter City ugenini, kocha Pellegrini alalamikia refari

Manuel Pellegrini, kocha wa klabu ya Manchester City
Manuel Pellegrini, kocha wa klabu ya Manchester City RFI

Barcelona ilianza vizuri michuano ya kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuifunga Manchester City mabao 2 kwa 0 katika uwanja wao nyumbani wa Etihad jumanne usiku.

Matangazo ya kibiashara

Bao la kwanza la Barcelona lilitiwa kimyani na mshambulizi Lionel Messi kupitia mkwaju wa Penati katika dakika ya 54 ya mchuano huo baada ya kuchezewa visivyo na mwargetina mwenzake Martín Gastón Demichelis amabye baadaye alipewa kadi nyekundu.

Bao la pili lilifungwa na Daniel Alves de Silva katika dakika ya 90 ya mchuano huo ambao Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema refarii kutoka Sweden Jonas Eriksson aliionea klabu yake.

Pellegrini ameeleza kuwa hakuona haja ya Demichelis kulambishwa kadi nyekundi na Barcelona kupewa Penalti kwa kile alichosisitiza kuwa mchuano wa jana Barcelona walionekana kuelemewa mno na vijana wake lakini walitafutiwa ushindi.

Matamshi ya pellegrini huenda yakamsababishia kupewa adhabu na shirkisho la soka barani Ulaya, baada ya kuonekana kumzomea na kumwambia mwamuzi huo kuwa alikuwa amefurahi kuwapa Barcelona ushindi.

Kufuzu kwa Manchester City ni lazima kuifunga Barcelona mabao 3 kwa 0 ugenini dhidi ya Barcelona katika mchuano wa mzunguko wa pili ili kuwa na matumaini ya kufika hatua ya robo fainali.

Katika mchuano mwingine, Paris Saint Germain ya Ufransa iliwafunga Bayer 04 Leverkusen ya ujerumani mabao 4 kwa 0 nyumbani kwao, huku mabao mawili yakifungwa na Zlatan Ibrahimovich , huku Blaise Matuidi na Yohan Cabaye wakipata bao 1 kila mmoja.

Michuano hii inaendelea jumatano usiku ambapo Intern Milan ya Italia watakuwa nyumbani kuchuana na Atletico De Madrid ya Uhispania, huku Arsenal wakiwa nyumbani katika uwanja wao wa nyumbani kumenyana na mabingwa watetezi wa taji hili Bayern Munich.

Arsenal na Bayern Muniuch walikutana katika hatua hii msimu uliopita na Bayern Munich walipata ushindi wa mabao 3 kwa 1 ugenini katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates na baadaye Arsenal wakapata ushindi wa mabao 2 kwa 0 mjini Munich na kushindwa kufuzu kutokana na ushindi wa ugenini.