MICHUANO YA KLABU BINGWA / ULAYA

Bayern Munich yatamba na kuibuka mshindi dhidi ya Arsenal

Furaha yaToni Kroos, lilpoifungia Bayer Munich bao la Kwnza
Furaha yaToni Kroos, lilpoifungia Bayer Munich bao la Kwnza Reuters

Mabingwa watetezi wa mchezo wa soka katika dimba la klabu bingwa barani Ulaya UEFA Bayern Munich ya Ujerumani waliandikisha matokeo ya kuridhisha jana usiku katika mchuano wa mzunguko wa kwanza wa kusakata nafasi ya kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Arsenal ya Uingereza mabao 2 kwa 0 katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Bayern Munich yalitiwa kimyani na kiungo wa kati Toni Kroos  katika dakika ya 54 ya mchuano huo na baadaye katika dakika ya 88 Thomas Müller akaipata timu yake bao la pili mbele ya maelfu ya maelfu wa Arsenal.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger na wachezaji wake watajilaumu wenyewe baada ya Mesut Ozil kukosa penalti ya wazi iliyookolewa na linda lango wa Bayern Munich Manuel Neuer.

Mlinda Lango wa Arsenal Szczesny Szczesny naye alilambiwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwnaza baad aya kumchezea ndivyo sivyo mshsmbulizi wa Bayern Munich Arjen Robben katika eneo la hatari.

Mchuano wa mzuguko wa pili utachezwa tarehe 11 mwezi ujao mjini Munich na Arsenal wanahitaji kuifunga Bayern Munich mabao 3 kwa 0 ili kujikatia tiketi ya kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Mbali na mchuano huo jijini London, Atletico Madrid ya Uhispania iliishinda AC Milan ya Italia bao 1 kwa 0 wakiwa ugenini katika uwanja wa San Siro.