BREZIL-Kombe la dunia

Usalama utaimarishwa na kuzingatiwa katika michuano ya Kombe la dunia 2014

Moja kati viwanja vitakavyopokea michuano ya kombe la dunia mwaka 2014, nchini Brazil
Moja kati viwanja vitakavyopokea michuano ya kombe la dunia mwaka 2014, nchini Brazil RFI

Serikali ya Brazil imetangaza kuwa polisi elfu sabini watataumiwa kulinda amani wakati wa kombe la dunia la mchezo wa soka mwezi juni mwaka huu. Zaidi ya mashabiki elfu 17 na wachezaji kutoka kote duniani wanatarajiwa kuwa nchini Brazil wakati wa michuano hiyo itakayochezwa katika miji 12.

Matangazo ya kibiashara

Rais Dilma Rousseff amesema kuwa maafisa wa usalama waliojihami kwa silaha pia watakuwa katika hali ya tadhari na watatumika ikiwa watalamika kufanya hivyo.

Tangu mwezi juni mwaka uliopita waandamani wamekuwa wakiandamana jijini Rio De Janeiro na miji mingine kulalamikia hali ya maisha nchini humo na kuzua hali ya wasiwasi kutokea kwa maandamano kama hayo wakati wa kombe la dunia.

Shirikisho la soka duniani FIFA ilikuwa imeomba Brazil kutumia maafisa 100,000 wa usalama wakati wa michuano hiyo na ongezeko la 200,000 limewapa tumaini la kuwepo kwa usalama wa hali ya juu wakati wa michuano hiyo.

Mbali na mswala ya usalama FIFA imekuwa ikilalamikia maandalizi duni ya michuano hiyo na hata kuonya kuwa huenda baadhi ya viwanja visikamilike kwa wakati kabla ya michuano hiyo kuanza lakini serikali ya Brazil imesema kuwa mambo yote yatakamilika kwa wakati kabla ya kuanza kwa dimba hilo.