footlball

Chelsea wajipa matumaini ya kusonga mbele michuano ya UEFA

PSG wakishangilia baada ya kuwachapa  Chelsea. 3x1.
PSG wakishangilia baada ya kuwachapa Chelsea. 3x1. REUTERS/Benoit Tessier

Mshambulzii wa Kimataifa wa Cameroon Samwel Eto'o huenda akaichezea klabu yake ya Chelsea itakayoshuka dimbani usiku huu kumenyana na klabu kutoka nchini Ufaransa ya Paris St Germain katika mchuano wa mzunguko wa pili wa robo fainali kutafuta nafasi ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Eto mwenye umri wa miaka 33 amekosa michuano mitatu baada ya kupata jeraha la mkono lakini alionekana akifanya mazoezi na wenzake hapo jana.

Chelsea wana imani kuwa watapata ushindi mkubwa hivi leo katika uwanja wao wa Stanford Bridge licha ya kupoteza kwa mabao 3 kwa 1 katika mchuano wa kwanza wiki iliyopita.

Klabu ya Paris Sainy Germain nao watamkosa mshmbuliaji wao Zlatan Ibrahimovich kutokana na jeraha la paja. Nafasi ya mchezaji huyo wa Kimataifa wa Sweden ambaye ameifungia klabu yake mabao 40 msimu huu itachukuliwa na Edison Cavani.

Mbali na mchuano huo mechi nyingine ambayo pia inasubiriwa kwa hamu nu kati ya Real Madrid ya Uhispani na Borrusia Dortmund ya Ujerumani.

Katika mchuano wa kwanza , Real Madrid walipata ushindi mkubwa kwa kupata mabao 3 kwa 0 nyumbani na Borrusia Dormund wanatumai kuwa watatumia uwanja wake wa nyumbani kuwabandua nje Real Madrid katika kinyang'anyiro hicho.

Kesho Alhamisi, mabingwa watetezi Bayern Munuch watakuwa nyumbani kumenyana na Mancheter United baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa kwanza nchini Uingereza.

Barcelona nao watakuwa ugenini kumenyana na Athletico Madrid vlabui vyote kutoka nchini Uhispania baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1juma lililopita.
Kufikia kesho usiku mashabiki wa soka duniani watakuwa wamefahamu ni vlabu gani viumefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.