KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Chile

Timu ya Taifa ya Chile
Timu ya Taifa ya Chile fifa.com

Imeshiriki mara 8, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 14 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Timu ya taifa ya Chile ni maarufu kama “La Roja” Ikiwa imeshiriki mara nane toka kuanza kwa michuano ya kombe la dunia, Chile iko kwenye nafasi ya nne toka kundi la timu za Amerika Kusini pamoja na Paraguay ambazo zimeshiriki mara nyingi zaidi kombe hili toka ukanda wao. Mara mwisho kufanya vema kwenye fainali hizi ni mwaka 1962 huku mwaka 1998 nchini Ufaransa na 2010 nchini Afrika Kusini ikimaliza kwenye kumi na sita bora. 

Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Chile “La Roja” yenyewe iko kwenye kundi B ikijumuishwa na timu za taifa za Uholanzi, Uhispania na Australia, bado hili ni moja kati ya kundi gumu kwenye michuano ya mwaka huu.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Washambuliaji kama Alexis Sanchez na Eduardo Vargas ni wachezaji wanaotegemewa kwenye safu ya ushambuliaji wa timu hii, wengine ni viungo Matias Fernandez na Arturo Vidal huku vijana kama Jean Beausejour na Marcelo Diaz wakitegemewa kuongeza makali kwenye timu hii.

Benchi la Ufundi.

Kocha mkuu wa timu hii ni Jorge Sampaoli.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Ilimaliza kwenye nafasi ya tatu mwaka 1962 kwenye fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Chile. Vijana chini ya umri chini ya miaka 17 nchini Japan mwaka 1993 ilimaliza kwenye nafasi ya tatu. Vijana chini ya umri wa miaka 20 nchini Canada mwaka 2007 na kumaliza kwenye nafasi ya tatu na pia michuano ya Olympic ya vijana mwaka 2000.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na Elias Figueroa, Ivan Zamorano na Marcelo Salas.