KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast

Timu ya Taifa ya Ivory Coast
Timu ya Taifa ya Ivory Coast fifa.com

Imeshiriki mara 2, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 21 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Timu ya taifa ya Ivory Coast maarufu barani Afrika kama “The Elephants” imeshiriki mara mbili kwenye fainali za kombe la dunia lakini mara zote imekuwa haifanyi vizuri kwa kuwa imeishia tu kwenye hatua ya makundi, na hii pengine ni kwasababu ya makundi ambayo imekuwa ikipangwa. Mwaka 2006 kwenye fainali zilizopigwa nchini Ujerumani, Ivory Coast ilipangwa na argentina, Uholanzi, Serbia na Montenegro na kumaliza kwenye nafasi ya tatu kama walivyofanya hivyo kwenye fainali za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini ambapo walipangiwa timu za Brazil, Ureno na jamhuri ya Korea. 

Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Ivory Coast “The elephants” iko kwenye kundi C ikijumuishwa pamoja na timu ya taifa ya Colombia, Ugiriki na Japan, wachambuzi wa mambo wanaona kuwa bado kundi hili ni gumu kwa timu ya Ivroy Coast na huenda kwa mara nyingien wakaishia kwenye hatua ya makundi.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Ivory Coast ni moja kati ya timu zilizosheheni wachezaji wanaocheza soka la kulipwa Ulaya, mfano ni washambuliaji wake kama Didier Drogba na Solomon Kalou ambao wanaunda muungano mzuri pale mbele, viungo kama Didier Zakora na Yaya Toure ni wachezaji muhimu wa timu hii, washambuliaji wa pembeni kama Gervinho mabeki kama Emmanuel Eboue na kolo Toure ni miongoni mwa wachezaji tegemezi kwenye timu hii.

Benchi la Ufundi.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast ni, Sabri Lamouchi.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Kushiriki fainali hizi mwaka 2006 nchini Ujerumani, Afrika Kusini mwaka 2010 na kuondolewa kwenye hatua ya makundi, Kombe la dunia kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 17 nchini Canada mwaka 1987 na kumaliza kwenye nafasi ya tatu, na pia kombe la shirikisho la FIFA nchini Saudi Arabia mwaka 1992 na kumaliza kwenye nafasi ya nne.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na Laurent Pokou, Youssouf Fofana na Joel Tieh.