KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Uruguay

Timu ya Taifa ya Uruguay
Timu ya Taifa ya Uruguay fifa.com

Imeshiriki mara 11, imetwaa taji hili mara 2, iko katika nafasi ya 5 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.Uruguay imekuwa moja kati ya timu za taifa ambazo zinatajwa kuwa bora zaidi duniani. Na historia yao ilijijenga baada ya kutwaa taji hili mara mbili kwa mtindo wa aina yake mwaka 1930 na mwaka 1950. Baada ya kushindwa kufuzu kwenye michuano ya mwaka 1994 nchini Marekani na mwaka 1998 nchini Ufaransa timu ya taifa ya Uruguay “La Celeste” ilirejea kwenye michuano ya mwaka 2002 nchini Japan na Korea na kutolewa kwenye hatua ya makundi. Walifuzu pia kwa bahati kwenye fainali za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini baada ya kuwafunga majirani zao Costa Rica kwenye mechi za kufuzu. 

Matangazo ya kibiashara

Kundi ililoko.

Timu ya taifa ya Uruguay iko kwenye D la michuano ya mwaka huu ya kombe la dunia pamoja na timu ya taifa ya Costa Rica, Uingereza na Italia, hili ni kundi jingine ambalo ili Uruguay ipite inahitaji kumfunga Uingereza, Italia na Costa Rica, hili waweza sema ni kundi la Kifo.

Wachezaji wa kuangaliwa.

Wako wachezaji wengi ambao Uruguay itajivunia kwenye mashindano ya mwaka huu kama vile mshambuliaji wa Liverpool ya Uingereza anayeoongoza kwa ufungaji, Louis Suarez na Edison Cavan wanatengeneza timu nzuri ya ushambuliaji kwa Uruguay. Fernando Muslera ni mlinda mlango anayetarajiwa kuwa tumaini la kuzuia mabao kwenye lango la timu yake ya taifa ya Uruguay.

Benchi la Ufundi.

Timu hii inaongozwa na kocha mkuu, Oscar Washington Tabarez.

Mafanikio pekee kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA.

Kushinda taji hili mwaka 1930 lilipofanyika kwenye ardhi yao, pia kushinda taji hili mwaka 1950 lilipofanyika nchini Brazil. Washindi wa kombe la Olympic mwaka 1924 jijini Paris Ufaransa na mwaka 1920 nchini Uholanzi. Washindi wa pili kwenye fainali za kombe la dunia kwa vijana wa chini ya miaka 17 mwaka 2011 nchini Mexico.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na Hector Scarone, Angel Romano, Obdulio Varela, Roque Maspoli, Alcides Ghiggia, Ladislao Mazurkiewicz, Pedro Rocha, Rodolfo Rodriguez, Hugo De Leon, Carlos Alberto Aguilera, Ruben Sosa, Enzo Francescoli na Alvaro Recoba.