FC BARCELONA

Fifa yairuhusu Barcelona kufanya usajili kwa muda huu ikisubiri uamuzi wa rufaa yake

Lionel Messi na Xavi Hernández wakipongezana baada ya ushindi wa timu yao hivi karibuni
Lionel Messi na Xavi Hernández wakipongezana baada ya ushindi wa timu yao hivi karibuni Reuters

Klabu ya Barcelona ya nchini Uhispania hatimaye imeruhusiwa kufanya usajili wakati wa dirisha dogo litakapofika barani Ulaya, ikisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake iliyoikata kwenye shirikisho la soka duniani FIFA.  

Matangazo ya kibiashara

Fifa awali ilitangaza kuifungia klabu hiyo kwa muda wa miezi 14 kutosajili mchezaji yeyote wakati wa dirisha dogo wala wakati wa msimu wa usajili kwa madai kuwa timu hiyo ilikiuka sheria za fifa za usajili wa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 18.

Hukumu hiyo ambayo ilionekana kuwamaliza kabisa FC Barcelona katika harakati zozote za kufanya usajili, ilikosolewa na baadhi ya wachambuzi wa soka na hata uongozi wa kalbu hiyo ambao uliona kana kwamba timu yao imeonewa.

Kufuatia hukumu hiyo iliyotolewa mwezi mmoja uliopita, uongozi wa Barcelona ulikata rufaa kwa shirikisho la soka fifa kupinga hukumu hiyo, ikieleza kwakina kuwa haikukiuka sheria za soka katika kusajili vijana wake.

Barcelona ambayo sasa inahaha kwenye ligi kuu ya soka ya Uhispania katika kuwania nafasi za juu za kwenye msimamo wa ligi na hata kutwaa kikombe, inakabiliwa na mapungufu ya wachezaji kadhaa ambao inabidi ifanye usajili wakati wa dirisha dogo la usajili.

Kwenye taarifa yake iliyochapishwa hii leo kwenye mtandao wa fifa.com na kwa klabu ya FC Barcelona, imetoa kibali kwa timu hiyo kufanya usajili wakati wa dirisha dogo wakati ikisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake iliyoikata kwenye shirikisho hilo.

Iwapo hukumu hiyo itaidhinishwa itashuhudia klabu hiyo ikishindwa kufanya usajili muhimu wakati wa dirisha dogola usajili na kwamba ingelazimika kusubiri kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitatu ndipo ifanye usajili hatua ambayo ingeathiri mwenendo wa timu hiyo.

Uamuzi huu wa fifa umekuja wakati muafaka, wakati huu klabu hii ikihusishwa na kutaka kufanya usajili wa kipa wa Borussia Monchengladbach ya Ujerumani, Marc-Andre ter Stegen na pia kutaka kumsajili kiungo Mcroatia Alen Halilovic.

Beki wa kati wa FB Barcelona, Carles Puyol ambaye ametangaza kuondoka mwishoni mwa msimu
Beki wa kati wa FB Barcelona, Carles Puyol ambaye ametangaza kuondoka mwishoni mwa msimu Reuters

Nahodha wa kitambo kwenye timu hiyo, Carles Puyol pamoja na mlinda mlango wao Victor Valdes wote kwa pamoja wametangaza kuachana na timu hiyo itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

 kuhusu usajili wa kimataifa zinaruhusu kufanya usajili kwa wachezaji walio na umri wa zaidi ya miaka 18.

Sheria hii inasema kuwa klabu inaweza kusajili mchezaji wa chini ya miaka 18 iwapo wazazi wa mchezaji huyo wamehamia kwenye nchi husika, pili iwapo wazazi wa mechazaji huyo wanatokea kwenye nchi za Ulaya na ukanda wa kiuchumi na tatu iwapo mchezaji wa umri wa miaka 16 na 18 anaishi umbali wa kilometa 100 toka makao makuu ya klabu hiyo.