LIGI KUU YA UHISPANIA

Atletico Madrid yajihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa wa Uhispania

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa REUTERS/Sergio Perez

Klabu ya Atletico Madrid ya nchini Uhispania mwishoni mwa juma ilijiweka kwenye mazingira mazuri zaidi ya kutwaa taji la ligi kuu nchini humo LA LIGA baada ya kupata ushindi dhidi ya Valencia.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji wa Atletico Madrid akijaribu kuwatoka wachezaji wa Chelsea
Mchezaji wa Atletico Madrid akijaribu kuwatoka wachezaji wa Chelsea REUTERS/Javier Barbancho

Bao lililofungwa na kiungo, Glanced Gabi lilitosha kuwapa ushindi vijana wanaoongozwa na kocha diego Simeone ambaye ni wazi amepania kutwaa taji la msimu huu.

Licha ya kumaliza ikiwa na wachezaji kumi uwanjani baada ya mchezaji Juanfran kutolewa na kadi nyekundu, haikuwafanya wachezaji wa Atletico kulisakama lango la wapinzani wao hadi walipopata goli.

Ushindi huu wa Atletico ni watisa mfululizo, ushindi ambao sasa unawaweka mbele kwa alama sita zaidi dhidi ya Real Madrid ambao nao walichomoza na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Osasuna.

Winga wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania, Cristiano Ronaldo
Winga wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania, Cristiano Ronaldo REUTERS/Paul Hanna

Los Rojiblancos kama wanavyofahamika wamebakiza michezo mitatu ambayo iwapo watashinda itawawezesha kutwaa taji hili huku mechi ya mwisho ikiwa ni dhidi ya FC Barcelona tarehe 18 May mwaka huu.

Huu utakuwa ni ubingwa wao wa kwanza toka mwaka 1996 walipofanya hivyo.

Vijana wa Simeone ambao Jumatano hii watasafiri hadi nchini Uingereza kuwakabili Chelsea kwenye mchuano wa klabu bingwa Ulaya, tarehe 4 ya mwezi May watakuwa na kibarua dhidi ya Lavente kabla ya May 11 kuwakaribisha nyumbani klabu ya Malaga.

Wachezaji wa timu ya FC Barcelona wakishangilia moja ya mabao waliyofunga
Wachezaji wa timu ya FC Barcelona wakishangilia moja ya mabao waliyofunga REUTERS/Albert Gea

Kwa matokeo ya mwishoni mwa juma, yanawafanya Atletico Madrid kuwa na alama 88, wakifuatiwa kwa ukaribu na FC Barcelona ambayo baada ya kushinda mchezo wake wa mwishoni mwa juma dhidi ya Villareal wamefikisha alama 84 mbele ya Real Madrid yenye alama 82 huku ikiwa na mchezo mmoja kibindoni.