LIGI YA URENO

Julen Lopetegui kocha mpya wa FC Porto

Mcezaji wa FC Porto, Maïcon (kushoto) akikabiliana Zlatan Ibrahimovic (PSG), kwenye uwanja wa Dragon  Porto.
Mcezaji wa FC Porto, Maïcon (kushoto) akikabiliana Zlatan Ibrahimovic (PSG), kwenye uwanja wa Dragon Porto. REUTERS/Miguel Vidal

Meneja wa klabu ya Espoir ya Uhispania Julen Lopetegui, amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya FC Porto ya Ureno, kiongozi wa klabu ya FC Porto, Jorge Pinto da Costa, amethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Uhispania, ambae aliwahi kua golikipa wa klabu ya Real Madrid na klabu ya Barcelona, alianza shughuli yake ya ukocha mwaka 2003, wakati huo akiinoa klabu ya Rayo Vallecano.

Lopetegui, mwenye umri wa miaka 47, alitwaa ubingwa barani Ulaya mara mbili mfululizo: mwaka 2011 akiinoa klabu ya Uhipania ya vijana waliyo na umri uliyo chini ya miaka 19, na baadae mwaka 2013, akiinoa timu ya vijana waliyo na umri uliyo chini ya miaka 21.

FC Porto haijafanya vizuri katika msimu uliyopita na kuchukua nafasi ya tatu katika ligi kuu ya Ureno, licha ya meneja wake, Paulo Fonseca kutimliwa, na nafasi yake ikachukuliwa na Luis Castro mwanzoni mwa mwezi wa machi.

FC Porto inachukua nafasi ya tatu ikiwa na alama 58, baada ya nafasi ya pili kuchukuliwa na Sporting Portugal ikiwa na alama 67, huku ligi ikiongozwa na Benfica ikiwa na alama74.