KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza chawekwa hadharani, makinda washeheni

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ambaye leo ametangaza kikosi chake
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ambaye leo ametangaza kikosi chake thefa.com

Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza hatimaye kimefahamika baada ya kutangazwa na kocha mkuu wa timu hiyo, mzawa Roy Hodgson ambaye amejumuisha wachezaji wengi wanaochipukia.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho ambacho kilikuwa kinasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa Uingereza, kimekata kiu ya mashabiki hao ambao wengi wameonekana kuunga mkono hatua ya kocha wao kuwajumuisha vijana wengie kwenye kikosi chake.

Kikosi hicho wametemwa wachezaji waliokuwa wakongwe kama Ashley Cole anayekipiga na Chelsea, John Terry pia wa Chelsea, Rio Ferdinand anayekipiga na Manchester United, wamo pia Michael Carrick na wengine.

Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wafuatao ambapo kwenye mabano ni timu ambazo wanacheza:

Walinda mlango ni, Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City).

Walinzi ni pamoja na, Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Luke Shaw (Southampton), Chris Smalling (Manchester United).

Viungo wanaounda timu hiyo ni pamoja na, Ross Barkley (Everton), Steven Gerrard (Liverpool), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Jack Wilshere (Arsenal).

Washambuliaji ni pamoja na, Rickie Lambert (Southampton), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).

Wachezaji wengine waliotajwa na kocha huyo kama wachezaji wake wa akiba kwenye orodha yake ni pamoja na, John Ruddy (Norwich City), Jon Flanagan (Liverpool), John Stones (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley (Manchester United), Andy Carroll (West Ham United), Jermain Defoe (Toronto FC).

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangaza kikosi hicho, kocha Roy Hodgson anasema kuwa wachezaji aliowajumuisha wametokana na kujituma kwao kwenye vilabu pamoja na mchango walioutoa.