KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Blatter: Ilikuwa makosa kuipa Qatar nafasi kuandaa fainali za 2022, asisitiza kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi wa mwaka 2015

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter amesema kuwa kuipa nchi ya Qatar nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 ilikuwa ni makosa na badala yake michuano hiyo ilipaswa kufanyika kipindi cha baridi.Blatter anatoa kauli hii wakati huu ambapo pia akitangaza kutetea kiti chake cha urais wa shirikisho hilo kwa muhula wa tano mfululizo akipingana na matamshi yake ya awali kuwa asingewania kiti hichi.

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani, Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani, Sepp Blatter fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Cheikh Tamim mwanamfalme wa Qatar akisalimiana na rais wa fifa, Sepp Blatter walipokutana mwezi November mwaka jana
Cheikh Tamim mwanamfalme wa Qatar akisalimiana na rais wa fifa, Sepp Blatter walipokutana mwezi November mwaka jana REUTERS/Fadi Al-Assaad

Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni nchini Uswis, rais Blatter alipoulizwa iwapo ilikuwa ni makosa kuipa nchi ya mashariki ya kati kuandaa fainali hizo ilikuwa ni makosa, alijibu kifupi kuwa "Ndio, ilikuwa makosa na kwamba kila mtu anajifunza kutokana na makosa". anasema Blatter.

Kauli ya Blatter inakuja wakati huu ambapo kumekuwa na maoni tofauti kuhusu fainali hizo kufanyika nchini Qatar, nchi ambayo wakati wa majira ya kipupwe nchi hiyo itakuwa na joto la hali ya juu linalokadiriwa kufikia nyuzi joto zaidi ya 40.

Mbali na hatari ya taifa hilo kuwa na joto jingi wakati wa fainali hizo, kumekuwa na shinikizo pia la kufanyika kwa uchunguzi kubaini iwapo nchi hiyo ilishinda kihalali nafasi ya kupewa kuandaa fainali hizo ama kulikuwa na mazingira ya rushwa.

Rais wa fifa, Sepp Blatter
Rais wa fifa, Sepp Blatter REUTERS/Ueslei Marcelino

Akijibu hoja hiyo, Blatter anasema kuwa licha ya kuwa kulikuwa na makosa yaliyofanyika wakati wa kutoa nafasi hiyo kwa Qatar, lakini ushindi wa Qatar haukuwa na chembe ya mazingira ya rushwa kama inavyodaiwa na baadhi ya nchi.

Rais huyu wa FIFA anasema kuwa kamati ya ufundi inayofuatilia matayarisho ya fainali hizi nchini Qatar ilipitia tena ripoti yake na kuondoa uwezekano kuwa huenda kipindi ambacho fainali hizi zinafanyika kati ya mwezi June na July nchi hiyo itakuwa na joto la hali ya juu.

Fifa imekosolewa kwa sehemu kubwa kutokana na hatua yake ya kuipa nchi ya Qatar nafasi ya kuandaa michuano hiyo ya mwaka 2022 kwa kile inachodaiwa kuwa wachezaji wengie wataathiriwa na hali ya joto itakayokuwepo nchini humo.

Rais wa FIFA, Sepp Blatter akionesha bahasha iliyoipa ushindi nchi ya Qatar kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022
Rais wa FIFA, Sepp Blatter akionesha bahasha iliyoipa ushindi nchi ya Qatar kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022 Reuters

Kuhusu kuwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo, Blatter anasema kuwa "Ndio ntawania tena muhula mwingine kwasababu bado nnauwezo na ninataka kuendelea pia", anasema Blatter.

Mwaka mmoja uliopita kiongozi huyu alinukuliwa na vyombo vya habari duniani akisema kuwa hatowania tena kiti hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, kauli ambayo sasa anaonekana kuikana.

Sepp Blatter amekuwa rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani toka mwaka 1998 ambapo mwaka 2011 alishinda kiti hicho bila kuwa na mpinzani.