MESSI-BARCELONA

Messi aafikiana na klabu yake ya Barcelona kufanya marekebisho kwenye mkataba wake

REUTERS/Albert Gea

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya FC Barcelona, Lionel Messi hatimaye amekubaliana na klabu yake kufanyia marekebisho mkataba wake ambao utashuhudia mchezaji huyo akiendelea kusalia kuwa mchezaji wa Barcelona. 

Matangazo ya kibiashara

Lionel Messi ambaye amekuwa mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo, atakuwa mchezaji anayelipwa gali zaidi duniani kutokana na marekebisho haya yatakayofanyika kwenye mkataba wake.

Kwenye mtandao wa klabu hiyo unasema kuwa "FC Barcelona imefikia makubaliano na Messi kufanya mabadiliko kwenye mkataba wake na kumfanya mchezaji huyo kuwa mchezaji wa kulipwa wa kwanza, mkataba ambao utatiwa saini katika siku chache zijazo". Viongozi wa timu hiyo wamesema kupitia mtandao wa klabu hiyo.

Mchezaji Lionel Messi akisikitika baada ya timu yake kupoteza moja mechi zake na Atletico Madrid
Mchezaji Lionel Messi akisikitika baada ya timu yake kupoteza moja mechi zake na Atletico Madrid REUTERS/Juan Medina

Iwapo Lionel Messi atatia saini mkataba huu utashuhudia akimpiku mpinzani wake anayekipiga na klabu ya Real Madrid, Christian Ronaldo kama mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.

Christian Ronaldo alisaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitano zaidi mwezi November mwaka jana, mkataba unaomfanya mchezaji huyo kuwa na mapato ya euro milioni 17 kwa mwaka sawa na dola milioni 23 za Marekani kwa mwaka.

Messi anatarajiwa kupokea kiasi cha Euro milioni 20 kwa mwaka ikiwa na nyongeza ya euro milioni 5 zitakazotokana na marupurupu ya kushinda mataji, kufunga magoli na kila atakapokuwa akiichezea klabu yake.

Lionel Messi, mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona
Lionel Messi, mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona REUTERS/Paul Hanna

Mbali na mkataba huo, Messi pia atashuhudia akipokea asilimia 100 ya mapato yatakayokuwa yakitokana na mauzo ama matumizi ya picha zake.

Iwapo mchezaji huyo atatia saini mkataba huo utamfanya asalie kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 201.

Messi anakubalia kufanya marekebisho ya mkataba wake wakati huu akijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kama nahodha wa timu hiyo kuwaongoza wenzake kwenye fainali za mwaka huu nchini Brazil.