TENNIS

Michuano ya Tennis ya French Open katika siku ya tatu

Andy Murray ambaye ameshinda mataji mawili makubwa likiwemo lile la Wimbledon msimu uliopita.
Andy Murray ambaye ameshinda mataji mawili makubwa likiwemo lile la Wimbledon msimu uliopita. REUTERS/Adam Hunger

Leo ni siku ya tatu ya michuano ya Tennis ya French Open inayoendelea jijini Paris na Mwingereza Andy Murray ambaye ameshinda mataji mawili makubwa likiwemo lile la Wimbledon msimu uliopita, atashuka dimbani kumenyana na Andrey Golubev, kutoka Kazakhstan kwa upande wa wanaume katika mchezo wake wa kwanza.

Matangazo ya kibiashara

Upande wa wanawake bingwa wa Australian Open Li Na ameanza kutafuta ubingwa katika michuano hii dhidi ya Kristina Mladenovic wa Ufaransa.

Baadhi ya matokeo ya michuano ya jana Stanislas Wawrinka raia wa Usiwisi

Stanislas Wawrinka akishinda katika fainali ya michuano ya "Australian Open" mwaka 2014.
Stanislas Wawrinka akishinda katika fainali ya michuano ya "Australian Open" mwaka 2014. REUTERS/Petar Kujundzic

alibanduliwa nje ya michuano hiyo katika mzunguko wa kwanza baada ya kufungwa na Mhispania Guillermo Garcia-Lopez kwa seti za 6-4, 5-7, 6-2, 6-0.

Rafael Nadal naye alimshinda Robby Ginepri wa Marekani kwa seti 6-0, 6-3, 6-0.

 

Mserbia Novak Djokovic akamfunga  João Sousa wa Ureno kwa seti 6-1, 6-2, 6-4.

Maria Sharapova kutoka Urusi amemshinda Ksenia Pervak.
Maria Sharapova kutoka Urusi amemshinda Ksenia Pervak. REUTERS/Alessandro Bianchi

Kwa upande wa wanawake, Maria Sharapova kutoka Urusi amemshinda Mrusi mwezake Ksenia Pervak kwa seti 6-1, 6-2.