TENNIS-French Open

Andy Murray afuzu kutinga mzunguko wa 3 French Open

Andy Murray raia wa Scotland amefuzu katika mzunguko wa tatu wa michuano ya Tennis ya French Open ambayo yanaingia katika siku ya sita hivi leo.

Andy Murray afuzu kuingia mzunguko wa tatu wa French Open
Andy Murray afuzu kuingia mzunguko wa tatu wa French Open REUTERS/Suzanne Plunkett
Matangazo ya kibiashara

Murray alifuzu baada ya kumfunga Muaustralia Marinko Matosevic kwa seti za 6-3,6-1,6-3.

Bingwa huyo wa michuano ya Wmbledon sasa atamenyana na Mjerumani Philipp Kochreiber kufuzu katika hatua ya kumi na sita bora.

Naye bingwa mtetezi Rafael Nadal alifuzu baada ya kumfunga Dominic Thiem Kutoka Australia kwa seti 6-2,6-2,6-3.

Agnieszka Radwanska atamenyana na Ajla Tomljanovic wakati Dmitry Tursunov raia wa Urusi akikabiliana na Roger Federer .

Paula Ormaechea wa Argentina atamkabili Maria Sharapova huku Milos Raonic wa Cannada akipambana na Gilles Simon.

Dominika Cibulkova atamkabili Samantha Stosur wa Australia wakati Marin Cilic akipambana na Novak Djokovic raia wa Serbia.

Jo-Wilfried Tsonga raia wa Ufaransa atamkabili Jerzy Janowicz raia wa Pland na Daniela Hantuchova akiumana na Angelique Kerber raia wa Ujerumani.