KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Kikosi rasmi cha timu ya taifa ya Colombia chatangazwa, huku Falcao akiachwa

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Colombia, Radamel Falcao ambaye atakosa fainali za kombe la dunia mwaka huu
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Colombia, Radamel Falcao ambaye atakosa fainali za kombe la dunia mwaka huu francetvinfo.fr

Mshambuliaji tegemo wa timu ya taifa ya Colombia, Radamel Falcao atakosa fainali za kombe la dunia la mwaka huu nchini Brazil baada ya kuachwa kwenye kikosi kamili cha timu yake kinachoelekea nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Jina la mchezaji huyo halikutajwa kwenye orodha ya wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Colombia watakaoelekea nchini Brazil tayari kwa michuano ya mwaka huu, baada ya kubainishwa rasmi kuwa hatoweza kucheza fainali za mwaka huu.

Falcao mwenye umri wa miaka 28 na anayekipiga na klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa hajaichezea timu yake toka alipopata jeraha la goti mwezi January mwaka huu.

Falcao licha ya kutocheza mecho yoyote kwenye timu yake na timu ya taifa lakini aijumuishwa na kocha wake, Jose Pekerman kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 30 kabla ya kutangaza kikosi rasmi cha wachezaji 23 wanaoenda nchini Brazili.

Radamel Falcao akiwa na jopo la madaktari waliomfanyia upasuaji mwezi January mwaka huu.
Radamel Falcao akiwa na jopo la madaktari waliomfanyia upasuaji mwezi January mwaka huu. @ASMFC_MONACO

Mshambuliaji huyu mwenye nguvu aliifungia timu yake mabao tisa wakati wa michuano ya kufuzu kuelekea nchini Brazil.

Wachezaji wengine ambao hawamo kwenye kikosi cha timu hii kinachoelekea nchini Brazil ni pamoja na mabeki, Aquivaldo Mosquera anayecheza kalbu ya America, Luis Amaranto Perea anayecheza na klabu ya Cruz Azul, viungo walioachwa ni pamoja na Macnelly Torres anayekipiga na klabu ya Al Shabab, Elkin Soto anayecheza Mainz, na Edwin Valencia anayekipiga na Fluminense, huku mshambuliaji wa Udinese Luis Fernando Muriel nae akiachwa.

Timu hii iko kwenye kundi C pamoja na timu ya Ugiriki, Ivory Coast na Japan.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Colombia kinaundwa na walinda mlango, David Ospina (Nice), Faryd Mondragon (Deportivo Cali), Camilo Vargas (Independiente Santa Fe).

safu ya Ulinzi inawajumuisha wachezaji, Mario Yepes (AC Milan), Cristian Zapata (AC Milan), Pablo Armero (West Ham, on loan from Napoli), Camilo Zuniga (Napoli), Santiago Arias (PSV Eindhoven), Eder Alvarez Balanta (River Plate), Carlos Valdes (San Lorenzo).

Viungo wataongozwa na, Fredy Guarin (Inter Milan), Juan Cuadrado (Fiorentina), James Rodriguez (Monaco), Abel Aguilar (Toulouse), Juan Fernando Quintero (Porto), Carlos Sanchez (Elche), Aldo Leao Ramirez (Morelia), Alexander Mejia (Atletico Nacional),

Na safu ya ushambuliaji sasa itaongozwa na wachezaji, Victor Ibarbo (Cagliari), Jackson Martinez (Porto), Carlos Bacca (Sevilla), Adrian Ramos (Hertha Berlin), Teofilo Gutierrez (River Plate).

Colombia itatupa karata yake ya kwanza June 14 kwenye mji wa Belo Horizonte na kisha tarehe 19 June kukutana na Ivory Coast kabla ya tarehe 24 June kucheza na Japan.