BRAZIL 2014

Shirikisho la soka la Uruguay kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Suarez

Beki wa Italia Giorgio Chiellini  baada ya kunga'twa na Suarez
Beki wa Italia Giorgio Chiellini baada ya kunga'twa na Suarez Foto: Reuters

Shirikisho la soka la Uruguay linasema litakata rufaa dhidi ya hatua iliyochukuliwa na Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka duniani  FIFA, kumpata na kosa mchezaji wake Luis Suarez kum'ngata beki wa Italia Giorgio Chiellini.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Shirikisho la soka la Uruguay Wilmer Valdez amewaambia waandishi wa habari jijini Rio de Janeiro, “ Tunashauriana na mawakili wetu na tunaenda kukata rufaa hivi leo.,”

“Tuna siku tatu kukata rufaa, na tunajitahidi kufanya hivyo,” aliongezea.

“Sisi tunaona hakuna ushahidi kuonesha kuwa adhabu aliyopewa Suarez inafaa. Hapa tunazungumzia kutocheza mechi tisa za Kimataifa, kutocheza miezi minne na kulipa faini, hii ni adhabu kali sana.,” alisisitiza.

Naye beki wa timu ya taifa ya Italia, Giorgio Chiellini anasema adhabu aliyopewa Suarez ya kutocheza mechi nne ni kali mno.

Chiellini, amesema “ Sina machungu na Suarez, wala sijiskii vizuri kwa sababu amefungiwa na FIFA, namruhumia.,”

Suárez  baada ya kum'ngata Chiellini
Suárez baada ya kum'ngata Chiellini REUTERS/Tony Gentile/Files

Suarez pia ameungwa mkono na mchezaji maarufu wa Argentina Diego Maradona,ambaye amesema adhabu dhidi ya Suarez ni aibu.

Suarez, anayechezea klabu ya Liverpool alirudi nchini Uruguay siku ya Ijumaa asubuhi na kupokelewa na maelfu ya wapenzi wa soka jijini Montevideo.

Mashabiki wa Suarez wakimsubiri katika uwanja wa Kimataufa wa  Montevideo
Mashabiki wa Suarez wakimsubiri katika uwanja wa Kimataufa wa Montevideo Reuters/Carlos Pazos

FIFA katika adhabu yake imemtoza Suarez faini ya Pauni 65,680 na kumpiga marufuku kucheza mechi 9 za Kimataifa.

Adhabu ya FIFA dhidi ya Suarez ndio ndefu na kubwa zaidi kuwahi kutolewa dhidi ya mchezaji katika historia ya kombe la dunia.

Kitendo cha Suarez kimemsabishia kusitishwa kwa ufadhili wa kampuni ya kucheza kamari katika mchezo wa soka 888poker iliyokuwa inafanya shughuli zake kwa jina lake.