BRAZIL 2014

Brazil na Colombia zafuzu hatua ya robo fainali

Neymar akifunga penalti dhidi ya Chile
Neymar akifunga penalti dhidi ya Chile REUTERS/Francois Xavier Marit/Pool

Brazil imefuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya soka ya kombe la dunia baada ya kuwashinda Chile kwa mabao 3 kwa 2 kupitia mikwaju ya penalti Jumamosi usiku.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo ulilazimika kufikia hatua ya kupigwa penalti baada ya timu zote mbili kutoka sare ya bao 1 kwa 1 katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

David Luiz aliipa Brazil bao la ufunguzi katika dakika ya 18 ya mchuano huo kabla ya Alexis Sanchez kuishawazishia timu yake katika dakika ya 32 .

Wachezaji wa Brazil wakishangilia baada ya kufuzu katika hatua ya robo fainali
Wachezaji wa Brazil wakishangilia baada ya kufuzu katika hatua ya robo fainali 路透社

Kipa wa Brazil Julio Cesar ndiye aliyekuwa mchezaji bora katika mchuano huo kwa kuikoa timu hiyo kwa kuokoa penalti mbili.

Kocha Luiz Felipe Scolari akimpa maelekezo Neymar
Kocha Luiz Felipe Scolari akimpa maelekezo Neymar Foto: Reuters

Cesar aliokoa penalti ya Mauricio Pinilla na Alexis Sanchez, huku wao Brazil wakifunga penalti 3 katika mchuano huo mgumu.

Penalti zilifungwa na David Luiz , Marcelo na Neymar.

Mashabiki wa Brazil
Mashabiki wa Brazil Elcio Ramalho/RFI

Mbali na Brazil, James Rodriguez wa Colombia  aliifungia timu yake mabao mawili katika dakika ya 28 na 50 na kuwabandua nje Uruguay katika michuano hii.

Rodriguez anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika kila mechi katika michuano hii na hadi sasa, ni mfugaji bora akiwa na mabao 5, akifuatwa na Neymar wa Brazil na Lionel Messi wa Argentina ambao wana mabao 4.

Cristian Rodriguez wa Uruguay akimenyana na   Juan Cuadrado wa Colombia
Cristian Rodriguez wa Uruguay akimenyana na Juan Cuadrado wa Colombia REUTERS/Kai Pfaffenbach

Diego Forian na Edinson Cavani wa Uruguay
Diego Forian na Edinson Cavani wa Uruguay

Hii ndio mara ya kwanza katika historia ya Colombia kufuzu katika hatua ya robo fainali.

Brazil itamenyana na Colombia katika hatua ya robo fainali, siku ya Ijumaa juma lijalo.