BRAZIL-Kombe la dunia

Brazili na Ujerumani mabingwa wawili wakutana

Brazili na Ujerumani mabingwa wawili wakutana.
Brazili na Ujerumani mabingwa wawili wakutana. REUTERS/Leonhard Foeger

Wenyeji Brazil wanacheza na Ujerumani katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali leo usiku. Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema vijana wake wataonesha mchezo wa hali ya juu licha ya kutokuwepo kwa mshambulizi anayetegemewa Neymar ambaye alipata jeraha la mgongo katika hatua ya robo fainali juma lilolopita.

Matangazo ya kibiashara

Scholari amesema wachezaji wake wako tayari kwa mchuano wa leo na Neymar yeye amekwisha toa mchango wake katika kikosi hicho.

Kikosi cha wachezaji 11 cha timu ya taifa ya Brazil.
Kikosi cha wachezaji 11 cha timu ya taifa ya Brazil. REUTERS/Eric Gaillard

Thiago Silva akipewa kadi ya pili ya manjano, na kadi hio ndio imemsababishia kutoshriki mchuano wa jumanne hii.
Thiago Silva akipewa kadi ya pili ya manjano, na kadi hio ndio imemsababishia kutoshriki mchuano wa jumanne hii. REUTERS/Yves Herman

Brazil pia watamkosa nahodha wao, Thiago Silva ambaye alipewa adhabu ya kucheza mechi ya leo kwa kucheza visivyo katika mchuano wa robo fainali.

Dante anatarajiwa kuwa nahodha kwa upande wa Brazil, huku Luis Gustavo ambaye amemaliza adhabu yake akirejea uwanjani hii leo.

 

Kwa upande wa Ujerumani kocha Joachim Low, atakuwa anawategemea wachezaji kama Miroslav Klose ambaye ataichezea timu yake kwa mara ya 23 leo , Thomas Muller, Mesut Ozil, Philip Lahm kupata mabao na kuwanyamazisha mashabiki wa Brazil nyumbani kwao.

Mchezaji wa winga ya kulia wa timu ya taifa ya Ufaransa, Mathieu Debuchy (kushoto) akikabiliana na  mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, Miroslav Klose.
Mchezaji wa winga ya kulia wa timu ya taifa ya Ufaransa, Mathieu Debuchy (kushoto) akikabiliana na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, Miroslav Klose. REUTERS/Morris Mac Matzen

Hii ni mara ya 13 kwa Ujerumani kufika katika hatua ya nusu fainali, na inakuwa timu ya kwanza kufika katika hatua hii mara nne mfululizo.

Katika nusu fainali 11 zilizopita, wameshinda nne na kupoteza tano na mechi mbilii wamelazimisha mikwajiu ya penalti baada ya kutoka sare ya kutofunganaa.

Katika historia ya michuano hii, Brazil wamefika katika hatua hii ya nusu fainali mara 11, na nusu fainali ya pekee waliowahi kupoteza ilikuwa ni mwaka 1938 dhidi ya Argentina.

Wameshinda mechi tano ya nusu fainali na kutoka sare mara moja.

Mara ya mwisho Brazil na Ujerumani kukutana ilikuwa ni wakati wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2002, fainali ambayo Brazil waliishinda Ujerumani mabao 2 kwa 0 mabao yote yalifungwa na Ronaldo.

Je, Ujerumani ambao wameshinda kombe la dunia mara tatu mara ya mwisho ikiwa mwaka 1990 watafanikiwa katika hatua hii ya nusu fainali labda ya fainali au itakuwa ni Brazil ambayo mashabiki wake wamekuwa wakifunga na kuomba kupata ushindi leo na kunyakua taji hili kwa mara ya sita ?

Dakika 90 au zaidi za refari ndizo zitakazoamua leo katika uwanja wa Estadio Mineirao, mjini Belo Horizonte kuanzia saa tano usiku saa za Afrika Mashariki sawa na saa nne usiku saa za Afrika ya kati.