BRAZIL 2014

Argentina yafuzu fainali

Wachezaji waArgentina  wakisherehekea baada ya kufuzu fainali
Wachezaji waArgentina wakisherehekea baada ya kufuzu fainali

Argentina itakutana na Ujerumani katika fainali ya michuano ya soka ya  kombe la dunia siku ya Jumapili nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Argentina ilifuzu baada ya kuifunga Uholanzi katika hatua ya nusu fainali  mabao 4 kwa 2 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote kumaliza mchuano huo bila ya kufungana.

Mataifa haya mawili yamewahi kukutana katika fainali ya michuano hii mwaka 1986 na 1990 mfululizo.

Mwaka 1986 Argentina iliifunga Ujerumani mabao 3 kwa 2 katika fainali iliyochezwa nchini Mexico na kunyakua ubingwa lakini mwaka 1990, Ujerumani waliifunga Argentina bao 1 kwa 0 wakati michuano hiyo ilipochezwa nchini Italia.

Mashabiki wa Argentina wakiwa mjini Buenos Aires.
Mashabiki wa Argentina wakiwa mjini Buenos Aires. REUTERS/Martin Acosta

Siku ya Jumatano, kipa wa Argentina Sergio Romero alikuwa kinara wa mechi hiyo baada ya kuzuia penalti mbili kutoka kwa wachezaji wa Uholanzi Ron Vlaar na Wesley Sneijder.

Kipa wa Argentina Sergio Romero
Kipa wa Argentina Sergio Romero 路透社

Hata hivyo, kipa wa Uholanzi Jasper Cillessen alishindwa kufikia rekodi ya kipa mwenzake Tim Krul aliyeikoa timu yake wakati wa michuano ya robo fainali wakati wa mikwaju ya penalti.

Robin van Persie akimenyana na wachezaji wa Argentina
Robin van Persie akimenyana na wachezaji wa Argentina REUTERS/Darren Staples

Ujerumani nayo ilifuzu siku ya Jumanne kwa kuifunga Brazil, wenyeweji wa michuano hii mabao 7 kwa 1.