UJERUMANI-Soka

Ujerumani : Miroslav Klose astaafu

Miroslav Klose, mchezaji wa kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani, akiwa pia pia mfungaji bora katika michuano ya kombe la dunia 2014, atangaza kuutaafu.
Miroslav Klose, mchezaji wa kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani, akiwa pia pia mfungaji bora katika michuano ya kombe la dunia 2014, atangaza kuutaafu. REUTERS/Mike Blake

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya ujerumani, Miroslav Klose, ambaye aliweka rekodi ya kihistoria kwa kuwa mfungaji bora katika michuano ya kombe la duni mwaka 2014, baada ya kufunga mabao 6 peke yake, ametangaza kuustaafu, shirikisho la soka la Ujerumani (DFB) limefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo wa klabu ya Lazio Rome, mwenye umri wa miaka 36, ameeleza kwamba anastaafu baada ya ndoto yake ya utotoni kukamilika, ikiwa ni pamoja na ushindi wa timu ya taifa ya ujerumani nchini Brazil, ambayo ilitwaa kombe la dunia. Klose amesema michuano hiyo ya kombe la dunia iliyompa sifa hatoisahau maishani mwake.

Klose ni mchezaji wa pili wa Mannschaft kutangaza kustaafu katika ngazi ya kimataifa baada ya ushindi wa timu ya taifa ya Ujerumani nchini Brazil. Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Philipp Lahm, mwenye umri wa miaka 30 alitangaza kustaafu siku 5 baada ya fainali kati ya Ujerumani na Argentina, jambo ambalo lilishangaza wengi.

Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora katika michuano ya kombe la dunia (mabao 16), ambayo ilikua inashikiliwa na Christian Ronaldo wa Brazil, ambaye alifunga mabao 15 kwenye guu lake katika michuano kama hiyo.

“Kwa kweli Miro, alionesha ujuzi wake na alitoa mchango mkubwa kwa timu ya taifa ya Ujerumani”, amesema cocha wa timu ya taifa ya ujerumani Joachim Löw, akibaini kwamba anaheshimu uamzi wa Miroslav na mchango aliotoa kwa timu ya taifa.

"Katika masuala ya soka na utu, tutamkumbuka Miroslov”, amemalizia Löw, akinukuliwa kwenye mtandao wa shirikisho la soka la Ujerumani (DFB).

Rais wa shirikisho la soka nchini Ujerumani, Wolfgang Niersbach, amebaini kwamba Klose hakua tu mchezaji tofauti na wengine, alikua pia mtu wa kuigwa.

“Kufuatia mabao 71 aliyofunga akiichezea timu ya taifa ya ujerumani na mabao 16 aliyofunga katika michuano ya kombe la dunia, ameweka rekodi mbili muhimu ambayo itampelekea kupata na fasi ya heshima katika kitabu cha kihistoria", amesema Niersbach.