SUPERCUP-UHISPANIA

Real Madrid na Atletico zaenda sare

Cristiano Ronaldo, akipewa tuzo ya mpira wa dhahabu mwaka 2013.
Cristiano Ronaldo, akipewa tuzo ya mpira wa dhahabu mwaka 2013. REUTERS/Arnd Wiegmann

Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, raia wa Ureno, ambaye hajawika msimu uliyopita, amelazimika kuondolewa nje ya uwanja, baada ya kupata jeraha la mguu katika michuano ya Supercup iliyoshirikisha Real Madrid dhidi ya Atletico.

Matangazo ya kibiashara

Hadi dakika ya mwisho ya mchezo timu hizo mbili zimelazimika kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Meneja wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti, ameelezea masikitiko yake kuona mchezaji wake anapata jeraha katika mzunguko wa kwanza mechi hizo, huku akiwa na matumaini kwamba, huenda akacheza mechi itakayofuata.

Cristiano Ronaldo, mchezaji aliyepata tuzo ya mpira wa dhahabu mara mbili ameondolea katika kipindi cha kwanza cha mchezo, nafasi yake ikachukuliwa na James Rodriguez, jambo ambalo limekua gumzo katika vyombo vya habari vya Uhispania, kusema kwamba jeraha hilo la mguu wavkushoto ndiyo liliyosababisha kutofanya vizuru msimu uliyopita.

“Amepata tatizo kwenye mguu wa kushoto. Hakua vizuri mwisho wa kipindi cha kwanza kutokana na jeraha hilo”, Ancelotti ameelezea vyombo vya habari, akibaini kwamba si tatizo kubwa.

Ronaldo alisumbuliwa kwa mara kadhaa wenye mguu wake wa kushoto katika kipindi chote cha msimu uliyopita, na kumsababishia kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu. Lakini mwishoni mwa mwezi Mei alirudi uwanjani, kabla ya kushiriki michuano ya kombe la dunia.