MICHUANO YA KOMBE LA BRAZIL

Klabu ya Gremio yafutwa katika michuno ya Kombe la Brazil

Mahakama Kuu ya michezo nchini Brazil, imechukua uamzi wa kufuta moja ya klabu nchini humo baada ya kundi moja la mashabiki wake kutoa matamshi machafu yenye lengo la kueneza chuki za kibaguzi.

Kikosi cha wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil.
Kikosi cha wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil. REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu ya michezo (TSJD) imechukua uamzi wa kuifuta katika michuano ya kombe la Brazil klabu ya Gremio de Porto Alegre, kutokana na machafuko yaliyosababishwa na matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na mashabiki wa klabu hiyo ilipokua ikichezea nyumbani jumatano wiki hii dhidi ya klabu ya Santos katika mzunguuko wa nane.

Hii ni kwa mara ya kwanza katika historia ya soka ulimwenguni, uamzi kama huo unachukuliwa, na wadadisi wanasema ingelikua mfano kwa shirikisho la soka duniani, FIFA.

Uamzi huo ulichukuliwa na jopu la majaji wa Mahakama Kuu ya michezo dhidi ya klabu ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Felipe Scolari. Hata hivo msemaji wa klabu hiyo amesema watakata rufaa.

Kundi moja la mashabuki wa klabu ya Gremio walitoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya golkipa wa santos, aranha, wakimfananisha na nyani.

Mkanda wa video ambao umechukuliwa kama ushahidi unaonesha jinsi shabiki mmoja mwanamke wa klabu ya Gremio akitamka mara kadhaa neno “Makako!” (nyani kwa lugha ya kireno) wakati golkipa huo anapookoa jahazi kwenye lango lake. Hali hiyo imesababisha hali ya sintofahamu nchini Brazil.

Mwanamke huyo alietoa matamshi hayo, ambae kwa sasa anafuatiliwa na vyomba vya sheria, amesikilizwa na polisi na baadae amefutwa kazi na muajiri wake.

Mbali na uamzi huo, Mahakama Kuu ya michezo imeitaka klabu ya Gremio kutoa faini ya pesa za kibrazil (Reais) 50,000 sawa na Uro 16,000.

Mashabiki waliyotoa matamshi hayo wamewekewa marufuku ya kutohudhuria mechi yoyote kwa muda wa miaka miwili.

Matamshi ya kibaguzi, hususan kelele za nyani na kitendo cha kutupa ndizi mbivu uwanjani vimekithiri katika viwanja mbalimbali barani Ulaya na Amerika Kusini, lakini baadhi ya vilabu vimekua vikitozwa faini.

Nchini Brazil, nusu ya raia milioni 200 wana asilia ya kiafrika.