MICHUANO YA MATAIFA BINGWA 2015

AFCON 2014: safari ya kufuzu Morroco 2014

Michuano ya soka baina ya mataifa ya Afrika kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Morroco inachezwa katika nchi mbalimbali barani Afrika siku ya Jumatano.

Michuano ya soka baina ya mataifa ya Afrika inachezwa katika nchi mbalimbali barani Afrika siku ya Jumatano.
Michuano ya soka baina ya mataifa ya Afrika inachezwa katika nchi mbalimbali barani Afrika siku ya Jumatano. P.Quillerier/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hii ni michuano ya pili ya makundi, baada ya mechi za kwanza kuchezwa mwanzoni mwa mwezi huu.

Kundi la A, Congo Brazil iliyopata ushindi wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Nigeria katika mchuano wa kwanza ugenini, wapo nyumbani kucheza na Sudan.

Nigeria ambayo imeponea chupuchupu kufungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA kutokana na mgogoro katika shirikisho lake la soka, itakuwa ugenini nchini Afrika Kusini kutafuta ushindi dhidi ya Bafana Bafana iliyopata ushindi wa mabao 3 kwa 0 dhidi ya Sudan.

Kundi la B, Malawi wako nyumbani kumenyana na Ethiopia, Algeria nao wako jijini Algiers kupambana na Mali.

Timu ya taifa ya Angola ambayo ipo katika kundi C, ipo jijini Luanda kucheza na Burkina Faso, huku Lesotho ikimaliza kazi na Gabon jijini Maseru.

Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo ipo katika kundi D, baada ya kufungwa na Cameroon juma liililopita nyumbani, itakuwa inasaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Sierra Leon.

Mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya miamba wa zamani Cameroon na Ivory Coast jijini Younde, kutokana na umahiri wa wachezaji wake, na pia hamu ya tizi mbili kutaka kufuzu na kunyakua taji hili.

Black Stars ya Ghana ipo ugenini mjini Lome, kupambana na Togo baada ya kushindwa kupata ushindi dhidi ya Uganda mwishhoni mwa juma lililopita mjini Kumasi.

Uganda ambayo iliinyima raha Ghana nyumbani kwao kwa kulazimisha sare ya bao 1 kwa 1, inamenyana na Guinea.

Kundi F, Msumbiji wanacheza na Niger jijini Maputo, huku visiwa vya Cape verde wakiwa nyumbani kucheza na Zambia ambayo ni mabingwa wa zamani wa soka barani Afrika.

Kundi G, Senegal imekwenda Gaborone nchini Bostwana kuendeleza ushindi wake baada ya kuishinda Misri mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa kwanza, huku Misri ikimenyana na waarabu wenzao Tunisia.

Washindi wa kwanza katika kila kundi, na atakayemaliza bora katika nafasi ya tatu atajiunga na Morroco wakati wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwakani.

Mabingwa watetezi ni Nigeria.