MICHEZO- KLABU BINGWA ULAYA

PSG kumenyana na Barcelona bila mshambuliaji wake machachari Ibrahimovic

David Luiz mchezaji wa  Paris Saint Germain,
David Luiz mchezaji wa Paris Saint Germain, REUTERS/Benoit Tessier

Klabu ya Ufaransa Paris Saint Germain hii leo usiku inashuka dimbani kwenye uwanja wa nyumbani kumenyana na Barcelona katika mechi ya kuwania ubingwa barani Ulaya. PSG inashuka uwanjani ikiwa na uhaba wa mshambuliaji wake machachari Zlatan Ibrahimovic.

Matangazo ya kibiashara

Klabu hizo mbili zinakutana baada ya kukutana katika mechi za robo fainali kuwania ubingwa msimu uliopita ambapo timu hizo zilitoka sarw ya kufungana mabao mawili kwa mawili katika mechi ya kwanza na bao moja kwa moja katika mechi ya marudio.

Mabao 10 kati ya 11 yaliopachikwa katika mechi 4 zilizopita za ligi ya mabingwa kati ya Barcelona na Paris Saint Germain zilipachikwa katika kipindi cha pili

PSG haijafungwa katika mechi 29 za mechi za awali ilizocheza ikiwa nyumbani, imeshinda mara 19 na kugawa mara 10.

Barcelona upande wake imeshinda pekee mechi 4 kati ya 13 ilizocheza ugenini katika ligi ya mabingwa, imegawa mara 3 na kufungwa mara 6.

Barcelona hijafungwa katika mechi zake za mwisho 9 ilizocheza na klabu kutoka Ufaransa, imeshinda mara 5 na kugawa mara 4, lakini mechi 4 kati ya 5 ilizocheza hivi karibuni imegawa.

Iwapo mchezaji wa Barcelona Xavi atacheza katika mechi hii ya leo jioni, atasherehekea mechi ya 143 ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, na kuvunja rikodi ya Raul Gonzalez aliecheza mechi 142.